Kenya: Upinzani umesisitiza msimamo wake kupinga muswada wa fedha wa 2023
NAIROBI – Wakati huu wabunge nchini Kenya, wakisubiri kusomwa mara ya tatu kwa muswada wa fedha ulioibua mjadala miongoni mwa raia na wadau nchini humo, muungano wa upinzani umesisitiza msimamo wake kupinga muswada huo inaosema utawaumiza wananchi.
Imechapishwa:
Muswada huu ulijadiliwa na kusomwa mara ya pili hapo jana Jumatano, ambapo wabunge walivutana kuhusu baadhi ya vipengele, licha ya Serikali kukubali kufanya marekebisho katika baadhi ya sehemu za muswada huo.
Miongoni mwa vipengele vinavyopingwa ni pamoja na kodi ya ujenzi wa makazi nafuu, nyongeza ya kodi katika mafuta na bidhaa nyingine ambazo zinamgusa mwananchi moja kwa moja, Serikali hata hivyo ikisisitiza muswada huo lazima upitishwe.
PRESS STATEMENT:
— Azimio TV (@AzimioTv) June 14, 2023
AZIMIO STAND ON REVISED FINANCE BILL, 20203:
1. We have had a meeting of Azimio Summit and the technical team regarding the inaugural budget estimates, including its so-called amendments that Kenya Kwanza moves for Second Reading in the National Assembly… pic.twitter.com/PMfuGAuClZ
Martha Karua, ni mwanasiasa kutoka muungano wa upinzani wa Azimio.
“Hakuna wakati Azimio imewatishia wabunge na baada ya bajeti hii ambayo ni rasimi haiuungwi mkono na Wakenya, azimio itachukua hatua zifaazo.” alisema Martha Karua.
Martha Karua- Mmoja wa viongozi wa upinzani nchini Kenya
Naye kiongozi wa muungano huo wa upinzani, Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga anasema atawaongoza raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki kupinga kupitishwa kwa Mswada wa Fedha wa 2023 .
Akizungumza wakati alipozuru soko la Toi katika eneo bunge la Kibra, jijiini Nairobi ambalo lilibomolewa lilichomeka mapema wiki hii, kiongozi huyo alikashifu masuala muhimu katika Mswada huo ikiwa ni pamoja na asilimia 16 ya ushuru wa bidhaa za petroli, ushuru wa nyumba, na fidia ya bima.
Upinzani umetoa wito kwa serikali kuaanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili kuhusu ushuru tata wa nyumba kwa nia ya kuwashawishi Wakenya kuunga mkono ajenda badala ya kuwashurutisha wafanyikazi na waajiri kulipa ushuru huo wa asilimia 1.5.