Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga aitaka serikali kuachana na muswada wa fedha wa 2023

NAIROBI – Nchini Kenya, kiongozi Azimio la Umoja  Raila Odinga ameongeza shinikizo kwa rais  William Ruto akimtaka  kuachana na mapendekezo ya muswada wa fedha wa mwaka wa 2023.

Upinzani unamtaka rais Ruto kuachana na muswada huo wa fedha wa 2023
Upinzani unamtaka rais Ruto kuachana na muswada huo wa fedha wa 2023 © Raila Odinga
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo mkongwe, ametoa wito kwa rais Ruto kuachana na mpango huo anaosema unalenga kuwaongezea wakenya mzigo  haswa wakati huu wanapokabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Muungano wa Azimio umetishia kutumia njia zengine ambazo zitawahusisha raia ikiwemo maandamano, iwapo rais Ruto atawashawishi wabunge kuunga mkono muswada huo.

Aidha katika hatua nyingine Odinga, ameishauri Serikali kupunguza ukubwa wa serikali, kuziba mianya inayochangia kupotea kwa fedha za umma, kupunguza safari za watumishi nje ya nchi, kupunguza marupurupu ya mawaziri na makatibu katika wizara.

Hizi majuzi rais Ruto alisema anasubiri kuona wabunge watakaopinga muswada huo, hatua ambayo wachambuzi wa siasa wanasema inalenga kuwashurutisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.