Pata taarifa kuu

Ghetto kids wa Uganda wameingia fainali ya Britain's Got Talent

NAIROBI – Kundi la watoto wasakata densi raia wa Uganda maarufu kama Ghetto Kids wamefanikiwa kufika kwenye fainali ya shindano maarufu la uhalisia la vipaji, Britain's Got Talent.

Wacheza densi kutoka nchini Uganda wamefika katika fainali za Britain's Got Talent
Wacheza densi kutoka nchini Uganda wamefika katika fainali za Britain's Got Talent © Triplets Ghetto Kids
Matangazo ya kibiashara

Watoto hao walipata mapokezi mazuri kutoka kwa majaji wote wanne wa shindano hilo baada kuonyesha mchezo mzuri na  kusisimua siku ya Jumatano usiku.

Kufuatia maonyesho hayo, waandaji Ant na Dec walizungumza na majaji Alesha Dixon na Simon Cowell wakachagua Ghetto Kids kutokana na mchezo wao bora.

Sita hao wenye umri wa miaka mitano hadi 13 ni yatima wanaoishi pamoja nchini Uganda baada ya kuasiliwa na baba yao Daouda Kavuma.

Watoto hao ni Priscila, 12, Asharif, 12, Akram, 13, Shakib, 12, Madwanah, 13 na Josephine, 5, ambao wamekuwa vipenzi vya mashabiki kutokana na shughuli zao za kila siku.

Watoto hao sita ni miongoni mwa mwengine 31 ambao Daouda amewapa makao baada ya kuwapata wakiishi kwenye maeneo hatari nchini Uganda.

 

Kwa kutumia densi kuwasaidia kutimiza uwezo wao, mwalimu huyo wa zamani wa shule ya msingi hadi sasa amebadilisha maisha ya takriban watoto 200.

Wengi wao wameenda kusoma katika chuo kikuu, wana taaluma zenye mafanikio au kuanzisha familia zao wenyewe. Fainali kuu ya Britain's Got Talent itaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumapili, 4 Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.