Pata taarifa kuu

Uganda: Marekani, watetezi wa haki za binadamu wapinga sheria mpya dhidi ya mashoga

NAIROBI – Nchini Uganda, saa chache baada ya rais Yoweri Museveni kutia saini sheria mpya, dhidi ya vitendo na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekwenda kwenye Mahakama ya Katiba, kuitaka kutupilia mbali sheria hiyo wanayosema inakiuka katiba ya nchi hiyo na ni katili.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Uganda kupinga sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Uganda kupinga sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo inaharamisha kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja lakini pia adhabu ya kifo intawakabili wvitendo vya mapenzi ya jinsia moja watakaowaambukiza wengine Ukimwi au kuwabaka watoto.

Huku haya yakijiri Rais wa Marekani Joe Biden, amelaani kutiwa saini kwa sheria hiyo na kutishia kukata misaada kwa nchi ya Uganda iwapo sheria hiyo haitabatilishwa.

Adrian Jjuuko ni mkurugenzi mtendaji wa  jukwaa la Uhamasishaji na Ukuzaji wa Haki za Binadamu nchini Uganda ni miongoni mwa watu wanaopinga sheria hiyo.

“Sheria hiyo ilipitishwa bila ushiriki wa kutosha na wa maana wa umma, Tuliona wakati mswada ulijadiliwa na kamati ya bunge hakuna hata mtu mmoja wa jinsia moja aliyeonekana kwa ajili ya kutoa maoni yake.” alisema Adrian Jjuuko.

00:40

Adrian Jjuuko kuhusu sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda

Aidha Adrian ameeleza kuwa mwenendo wa spika ulionyesha wazi upendeleo kwa sababu alitoa kauli zilizoonyesha wazi kuwa anaunga mkono kupitisha sheria hiyo lakini pia spika anatakiwa kutokuwa na upendeleo.

Marekani imefutilia mbali visa vya Spika wa Bunge nchini humo, Anita Among huku mbunge Asuman Basalirwa akisema yeye ndiye mwathiriwa wa kwanza wa uwezekano wa kuwekewa vikwazo baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo.

Chini ya sheria mpya, wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanakabiliwa na adhabu kali ambazo zinaweza kujumuisha kifungo cha maisha.

Mapema Jumatatu, Among alikuwa ameweka wazi kwamba "Bunge litasimamia na kuendeleza maslahi ya watu wa Uganda daima."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.