Pata taarifa kuu

Kenya: Maandamano ya upinzani kurejelewa hivi leo Jumanne

NAIROBI – Maeneo kadhaa ya nchi ya Kenya, hivi leo yanatarajia kushuhudia maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye hapo jana aliwataka wafuasi wake kujitokeza mapema licha ya katazo la idara ya polisi.

Polisi walikabiliana vikali na waandamanaji katika maandamano ya awali.
Polisi walikabiliana vikali na waandamanaji katika maandamano ya awali. REUTERS - JAMES KEYI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Odinga, polisi hawana mamlaka ya kuzuia kile alichosema maandamano ya amani, kiongozi huyo na wandani wake wakiahidi kuendelea kuweka shinikizo kwa utawala wa rais William Ruto.

DR Brian Mutie, ni mchambuzi wa masuala ya siasa, anaangazia kinachoendelea nchini Kenya.

“Nchini Kenya sio rahisi kufanyika kwa maandamano ya amani kwa sababu kama desturi yetu wakenya ni kwamba maandamano huja na mambo mengi yakiwemo uharibifu wa mali.” alisema DR Brian Mutie.

00:45

Brian Mutie kuhusu maandamano ya upinzani nchini Kenya

Odinga amesisitiza kile alichosema ni serikali kutaka kuwafunga mdomo raia huku nchi ikipitia changamoto zinazohitaji kushughulikiwa haraka, ikiwemo masuala ya rushwa, ukabila, gharama ya maisha na kuibuka kwa makanisha yenye utata.

Upinzani unaituhumu serikali kwa kupanda kwa  bei za bidhaa
Upinzani unaituhumu serikali kwa kupanda kwa bei za bidhaa AFP - YASUYOSHI CHIBA

Wakati Wanasiasa hao wakijiandaa kuandamana, idara ya polisi mapema wiki hii ilitoa onyo kwa viongozi hao ikipiga marufuku maandamano yoyote, huku ikiahidi kukabiliana vilivyo na watakaojitokeza, onyo ambalo tayari limezua mjadala.

Polisi wanasema kuwa maandamano ya awali yalisababisha vifo vya raia pamoja na kushuhudiwa kwa uharibifu wa mali ya raia, biashara zikitatizika wakati wa maandamano hayo.

Maandamano ya upinzani yaliofanyika awali katika mitaa ya jiji kuu la Nairobi
Maandamano ya upinzani yaliofanyika awali katika mitaa ya jiji kuu la Nairobi AP - Brian Inganga

Viongozi hao wawili siku za hapo nyuma walikubaliana kusitishwa kwa maandamano na kufanyika mazungumzo ya mapatano kupitia bunge, mazungumzo ambayo yameendelea kusuasua.

Jumatatu ya wiki akiongoza wakenya kuadhimisha sherehe hizo wa leba, rais William Ruto alisema serikali itanya iwezavyo kuzuia uharibifu wa mali na kuathirika shughuli za kiuchumi wakati wa maandamano.

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa serikali yake haitaruhusu maandamano ya kuharibu mali ya raia na kutatiza biashara
Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa serikali yake haitaruhusu maandamano ya kuharibu mali ya raia na kutatiza biashara REUTERS - MONICAH MWANGI

Maandamano haya yanaenda kufanyika huku kamati za wabunge kutoka pande zinazozozana, wakiendelea kuvutana, kitendo kinachodhihirisha kuwa huenda kusipatikane muafaka licha ya mwito wa rais Ruto na Odinga mwenyewe.

Hadi tukichapisha taarifa hii hakujaripotiwa maandamano yoyote makubwa, huku kukiwa na hofu ya kutokea makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi ila katika maeneo kadhaa vyombo vya habari vya ndani vimechapisha picha za baadhi ya waandamanaji wakichoma moto matairi ya magari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.