Pata taarifa kuu

Vita vya maneno kati ya rais Ruto na Raila kuhusu mazungumzo ya kisiasa

Serikali na upinzani nchini Kenya, wameendelea kusalia na misimamo mikali kuhusu mazungumzo ya kupata mwafaka kutokana na  mapendekezo walioyatoa wiki iliyopita.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na Naibu rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Cheche za maneno kati ya rais William Ruto na mpinzani wake Raila Odinga zinazidi kuonekana kila kukicha.

Siku ya Alhamisi, rais Ruto amesema kuwa Kinara wa upinzani Raila Odinga anaweza kukubali mazungumzo ya pande mbili kupitia Bunge au asubiri hadi uchaguzi mkuu wa 2027.

Mwishoni mwa juma lililopita, Raila aliitikia wito wa Ruto wa kusitisha maandamano, ili kuruhusu mazungumzo.

Nyinyi kama viongozi, tuendeni kule bunge tuongee maneno ya viongozi kule bunge. Tumewalipa mshahara, wabunge wako bungeni kuzungumzia sheria inayotaka kubadilishwa. Amesema Ruto.
00:19

Ruto kuhusu misimamo mikali

Kwa upande wake odinga naye anasema kuwa katiba ya mwaka 2010 inafaa kubadilishwa ili mshindi katika kiti cha urais asikuwe mamlaka yote.

Tunasukumwa na wasiwasi kwamba licha ya katiba ya mwaka 2010, utamaduni wetu wa kisiasa unabaki kuwa mshindi anakuwa na mamlaka ya kila kitu. Hii ndio imeonyeshwa wazi katika utawala uliopita. Amesema Raila.
00:22

Raila Odinga kuhusu katiba

Na huku mjadala ukisibiriwa bungeni, wananchi bado hawana imani na mchakato huo wa bungeni.

Kauli ya rais kusema gharama ya maisha ijadiliwe bungeni, sioni kama inafaa kwa sababu ukiangalia bungeni upande wa walio wengi ni serikali. Amesema mmoja wa raia.
01:14

Raia kuhusu mazungumzo haya

Rais Ruto, ameonya kuwa hatatekwa kisiasa, akisema viongozi wa Azimio wanapaswa wanapaswa kuzingatia hali ya kisiasa nchini, miezi saba tu baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 2022.

Naye Odinga amesema huenda mchakato wa bunge usishughulikie matatizo yao na kupendekeza zaidi kubuniwa kwa timu sawa na ile ya mkataba wa Kitaifa wa 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.