Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga atoa masharti mapya kuhusu mazungumzo

NAIROBI – Nchini Kenya, siku chache baada ya serikali na upinzani kukubaliana kutumia mazungumzo kutatua tofauti zao, muundo wa mazungumzo hayo, umezua mgawanyiko.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga na Rais William Ruto.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga na Rais William Ruto. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Jumapili iliyopita, rais William Ruto alitangaza utayari wa kuwa na mazungumzo na mpinzani wake mkuu wa kisiasa Raila Odinga kupitia bunge, kutatua malalamishi ya wapinzani, yaliyozua maandamano ya wiki mbili.

Hata hivyo, Odinga ambaye alikubali mazungumzo na kusitisha maandamano, amejitokeza na kusema kuwa, mazungumzo kupitia bunge, hayawezi kuzaa matunda.

Kiongozi huyo wa Azimio la Umoja sasa, anataka Kamati maalum itakayoundwa, iwe na mazungumzo ya kitaifa kama yale yaliyofanyika mwaka 2008 wakati nchi hiyo ilipoingia kwenye machafuko makubwa ya kisiasa.

Aidha, ameonya kuwa iwapo sharti hilo halitatekelezwa ataitisha maandamano mapya. Masuala anayotaka yashughulikiwe ni pamoja na kupunguza gharama ya maisha, kufungua mitambo iliyohifadhi matokeo ya urais ya mwaka uliopita, na Tume ya uchaguzi kufanyiwa mageuzi.

Muungano ulio madarakani wa Kenya Kwanza, unapinga sharti hilo la Odinga kwa madai kuwa mwanasiasa huyo mkongwe anatafuta mbinu ya kuundwa kwa serikali ya muungano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.