Pata taarifa kuu

Kenya: Upinzani wasitisha maandamano ya leo Jumatatu

NAIROBI – Kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, hapo jana Jumapili alitangaza kusitisha maandamano yaliyopangwa kufanyika hivi leo, akisema anatoa nafasi ya mazungumzo na Serikali baada ya karibu wiki mbili za maandamano yaliyoshuhudia vurugu.

 Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya
Raila Odinga, Kinara wa upinzani nchini Kenya REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Haya yametokea baada ya hotuba ya hapo jana ya rais William Ruto, kwa taifa ambapo alisema yuko tayari kuzungumza na wapinzani wake.

“Nimesikiliza kwa makini masuala yalioibuliwa na rafiki yangu Raila Odinga na nyakati kama hizi sio wakati wa kuangalia nani yuko sahihi au nani amekosea.”alisema Rais William Ruto.

 

00:37

William Ruto kuhusu mazungumzo nchini Kenya

Kufuatia kauli hiyo, baadae Raila Odinga na viongozi wengine, walijibu wito wa Ruto kwa kukubali kusitisha kwa muda maandamano yao ili kutoa nafasi ya majadilino lakini hata hivyo kwa masharti.

“Sisi tuko tayari kwa mazungumzo na tutaendelea kufanya hivyo kama ndugu Ruto na timu yake wako tayari.”alisema Raila Odinga.

 

00:32

Raila Odinga, Kuhusu mazungumzo nchini Kenya

Hatua hii tayari imepongezwa na wadau wa ndani na wale wa kimataifa ambao kwa majuma kadhaa wamekuwa wakiwashinikiza viongozi hao kuketi na kusikilizana ili kupata suluhu ya tofauti zao.

Maandamano ya wiki mbili sasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali, mamia ya raia wakiripotiwa kujeruhiwa wakiwemo maofisa ya polisi.

Awali  rais  William Ruto katika hotuba yake kwa taifa alikuwa ametoa wito  kiongozi wa upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano ya kesho na kukubaliana na mojawapo ya matakwa ya Bw Odinga ushirikiano wa pande mbili bungeni kuhusu kuundwa kwa tume mpya ya uchaguzi, IEBC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.