Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi watakiwa kueleza hatua walizochukua dhidi ya walioshambulia wanahabari

NAIROBI – Shirikisho la wanahabari nchini Kenya, limetoa siku 7 kwa ofisi ya mwendesha mashtaka kutoa taarifa kuhusu hatua walizochukua katika kuwafungulia mashtaka polisi na watu waliohusika kuwashambulia na kupora vifaa vya kazi kwa waandishi waliokuwa wakiripoti maandamano yaliyoitishwa na upinzani.

Polisi na waandamanaji nchini Kenya wameshutumiwa kwa kuwashmabulia wanahabari wakati wa maadamano
Polisi na waandamanaji nchini Kenya wameshutumiwa kwa kuwashmabulia wanahabari wakati wa maadamano Β© REUTERS - JAMES KEYI
Matangazo ya kibiashara

Kauli yao imekuja saa chache tangu wanasiasa wa mrengo wa chama tawala, mwishoni mwa juma lililopita, kutoa matamshi yaliyotafsiriwa kama kitisho kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Erick Oduor ni katibu mkuu wa shirikisho hilo.

β€œTuna ujumbe kwa mwendesha kutueleza ni hatua zipi wamechukua dhidi ya watu waliowashambulia na kuharibu vifa vya wanahabari, tunawapa siku saba kufanya hivyo.”alisema Erick Oduor.
00:29

Erick Oduor, katibu mkuu Shirikisho la wanahabari nchini Kenya

Katika hatua nyingine, rais William Ruto, amesisitiza serikali yake kutounga mkono vitendo vyovyote vinavyotishia uhuru wa habari, akisema wataendelea kutoa ushirikiano.

Β 

β€œSisi tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari na hivyo kitendo chochote ambacho kitamueka mwanahabari katika hatari hakikubaliki.”alisisitiza rais William Ruto.
00:26

William Ruto kuhusu uhuru wa wanahabari

Wanahabari wameripotiwa kujeruhiwa na vifa vyao vya kazi kuharibiwa na waandamanaji na maofisa wa polisi wakati walipokuwa katika harakati zao za kila siku za kuangazia maadamano ya upinzani nchini kenya.

Β 

Β 

Tayari kinara wa upinzani nchini kenya, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga amesitisha maandamano yaliokuwa yamepangwa kufanyika siku ya Jumatatu ya leo kama njia moja ya kutoa nafasi ya kufanyika kwa mazungumzo na serikali ya rais William Ruto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.