Pata taarifa kuu

Kenya :Marekani yatoa wito wa kuheshimu haki ya watu kufanya maandamano ya amani

NAIROBI – Nchini Kenya, wito wa utulivu unatolewa kufuatia vurugu na uharibifu wa mali, ambao umekuwa ukishuhudiwa wakati wa maandamano ya upinzani, ambayo pia yamepangwa kufanyika leo Alhamis.

Marekani yatoa wito wa kuheshimu haki ya watu kufanya maandamano ya amani nchini Kenya
Marekani yatoa wito wa kuheshimu haki ya watu kufanya maandamano ya amani nchini Kenya © Ben Curtis / AP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Umoja wa Afrika kutoa wito huo wiki hii baada ya maandamano ya Jumatatu, Mabalozi kutoka nchi Sita za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, zimeonesha wasiwasi wao na kutaka kuwepo kwa maridhiano kati ya rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Aidha, Mabalozi hao wamekaribisha hatua ya Polisi kusema kuwa, itachunguza waliovamia shamba la rais wa zamani Uhuru Kenyatta na kampuni ya Odinga wakati wa maandamano ya Jumatatu.

Odinga licha ya kukutana na  kufanya mazungumzo na Seneta wa Marekani Chris Coons pamoja na Masskofu wa Kanisa Katoliki hapo jana Jumatano amesema maandamano ya leo yataendelea, kushinikiza kushuka kwa gharama ya maisha na kudai kile anachosema haki ya uchaguzi wa mwaka uliopita.

Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Vedant Patel amevihimiza vyombo vya usalama kujizuia wakati wanapotekeleza majukumu ya kuwalinda raia na mali.

George Musamali ni mtaalama wa masuala ya usalama akiwa nchini Kenya hapa alihojiwa na mwandishi wetu Minzilet Ijai kuhusu suala hili.

"Marekani wanauwezo wa kupata taarifa za awali kwa sababu kuna wajasusi wengi sana wa Marekani katika mataifa ya bara Afrika haswa Kenya kwa sababu kuna masilahi yao mengi haswa nchini Kenya."ameeleza George Musamali.

02:27

Uchambuzi wake George Musamali kuhusu thadhari ya Marekani nchini Kenya

Rais William Ruto ambaye anazuru Ubelgiji amekuwa akilaani maandamano ya upinzani yaliyoharamishwa na polisi na kutaka kila mmoja kuuta sheria nchini humo.

Maandamano haya ya upinzani yamesababisha baadhi ya Shule nchini humo hasa jijini Nairobi kufungwa na wanafunzi kusalia nyumbani kwa kuhofia usalama wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.