Pata taarifa kuu
DRC - Siasa

DRC : Miaka 25 baada ya utawala wa Mobutu kuangushwa

Raia wa DRC, wanaadimisha miaka 25 tangu kuanguka kwa utawala wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mobutu Seses Seko.

Rais wa zamani wa DRC, Mobutu seseko
Rais wa zamani wa DRC, Mobutu seseko © rfi
Matangazo ya kibiashara

Mobutu aliongoza DRC, wakati huo ikijulikana kama Zaire, kwa zaidi ya miaka 30, kabla kuondoka jijini Kinshasa tarehe 17 Mei mwaka 1997, wakati waasi wakiongozwa na Laurent Kabila, walichukuwa madaraka na kubadili jina la taifa hilo kutoka Zaire , na kuliita Jumhuri ya Demokrasia ya Congo.

Mobutu aliyekimbilia uhamishoni nchini Morocco, baadaye alifariki na kuzikwa nchini humo.

Mwaka 2013, rais mustaafu wa DRC, Joseph Kabila, aliashiria mpango wa serikali kurejesha mabaki ya Mobutu nchini DRC, ila hilo halijafanyika hadi leo.

Wakosowaji wa Mobutu wanamhusisha na uongozi wa kimla, ufisadi na mauwaji ya waliopinga utawala wake, mbali na kutumia madini ya DRC kwa manufaa yake.

Mei 17 kila mwaka nchini DRC ni siku ya kitaifa, taifa likisherekea wanajeshi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.