Serikali ya DRC na makundi ya waasi kukutana Nairobi
Kenya itakuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na serikali ya Kinshasa
Imechapishwa:
Hili limeafikiwa baada ya mkutano wa viongozi wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kukutana siku ya Alhamisi jijini Nairobi, kujadili hali ya usalama mashariki mwa DRC.
Baada ya mkutano huo, serikali ya DRC ikiongozwa na rais Felix Tshisekedi, inatarajiwa kukutana na makundi ya waasi jijini Nairobi hivi leo.
Mazungumzo haya yanakuja karibu mwezi mmoja baada ya DRC kujumuishwa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, viongozi wa nchi hizo pia wamekubaliana kuangalia uwezekano wa kuunda jeshi la pamoja kukabiliana na makundi ya waasi iwapo yataendelea na harakati zao Mashariki mwa DRC.