Pata taarifa kuu

DRC: Felix Tshisekedi atia saini mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

DRC imetia saini rasmi Ijumaa, Aprili 8, mjini Nairobi, nchini Kenya, kujiunga katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Nchi hii ilikuwa imeomba kujiunga na jumuiya hiyo mwaka wa 2019. Leo asubuhi jijini Nairobi, Felix Tshisekedi aliidhinisha uanachama wa nchi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Uhuru Kenyatta (wa pili kulia) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (kushoto) wakiangalia uwakilishi mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye ramani baada ya kutia saini mkataba wa kuiunganisha DRC katika jumuiya ya kibiashara ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi mnamo Aprili 8, 2022.
Rais Uhuru Kenyatta (wa pili kulia) na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi (kushoto) wakiangalia uwakilishi mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye ramani baada ya kutia saini mkataba wa kuiunganisha DRC katika jumuiya ya kibiashara ya Afrika Mashariki, jijini Nairobi mnamo Aprili 8, 2022. AFP - TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Hafla rasmi ambayo ilifanyika mbele ya Mkuu wa Nchi ya Kenya, Uhuru Kenyatta, rais wa sasa wa jumuiya hiyo, pamoja na viongozi wenzake wa Uganda na Rwanda, Yoweri Museveni na Paul Kagame. Fursa kwa Wakuu wa Nchi waliopo kukumbusha matarajio ya jumuiya: kuwa na soko la pamoja na usafirishaji huru wa bidhaa na watu, lakini pia kuhimiza usalama katika eneo hilo.

Upatikanaji wa pwani ya Afrika Magharibi, uchumi wa watu milioni 90 na nchi tajiri kwa rasilimali. DRC inaleta fursa mpya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Akiongea kwanza, Uhuru Kenyatta hakuficha azma yake: “Sasa tuna jumuiya kubwa kama Ulaya, yenye takriban wakaazi sawa, rasilimali nyingi, wafanyakazi waliofunzwa... Tunazungumza lugha moja, tamaduni zilezile… mambo pekee yanayotutofautisha ni mipaka tuliyorithi toka enzi ya ukoloni. Hakuna sababu, ikiwa tunafanya kazi pamoja, kwamba hatuna nguvu na ustawi zaidi kiuchumi kuliko Ulaya au jumuiya yoyote ya kikanda. »

Felix Tshisekedi pia amekaribisha fursa hii ya kiuchumi. Huku akisisitiza haja ya kuwepo kwa utulivu katika eneo hilo: "Kwa kujiunga na jumuiya, watu wa Kongo hawataki tu kuridhika na manufaa ya biashara ya ndani ya jumuiya, lakini wanatamani kwanza kabisa kudumisha uhusiano unaozingatia amani na usalama kwa wote. Katika hali hii, watu wa Kongo wanarudia ahadi yao kwa sera ya ujirani mwema. Inatarajia kutoka kwa watu wengine kujitolea sawa kwa amani na usalama kwa wote. »

DRC sasa ina miezi sita kuweka taratibu zinazohusiana na uanachama wake.

Kenya na DRC pia zilitia saini Ijumaa makubaliano ya ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za kilimo, mifugo na uvuvi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.