Pata taarifa kuu
UFARANSA-HAKI

Mshukiwa wa mauaji ya Rwanda afanyiwa uchunguzi Paris

Isaac Kamali, anayeshukiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Watutsi, alishtakiwa Alhamisi kwa "mauaji ya kimbari" na "uhalifu dhidi ya binadamu", na kuwekwa chini ya udhibiti wa mahakama. Kulingana na mwendesha mashtaka wa kitaifa wa kupambana na ugaidi, amepinga madai hayo dhidi yake.

Watu zaidi ya laki nane kutoka jamii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.
Watu zaidi ya laki nane kutoka jamii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Mwanamume huyo aliyezaliwa nchini Rwanda mnamo mwaka 1949, anayeshukiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya Watutsi, alishtakiwa Alhamisi na hakimu wa uchunguzi wa Paris, nchini Ufaransa, hasa kwa "mauaji ya kimbari" na "uhalifu dhidi ya binadamu", imesema ofisi ya mashtaka dhidi ya Ugaidi (PNAT) . Isaac Kamali ambaye anakabilwa na uchunguzi wa kimahakama uliofunguliwa mnamo mwaka 2009, aliwekwa chini ya udhibiti wa mahakama.

Kulingana na taarifa ya PNAT kwa vyombo vya habari, ambayo inathibitisha habari kutoka kwa Gazeti la Parisien, Isaac Kamali anatuhumiwa kwa "kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari ya Watutsi yaliyofanywa nchini Rwanda mnamo mwaka 1994, hasa katika mkoa wa Gitarama".

Mahakama ya Rwanda yatoa hukumu ya kifo dhidi ya mshtumiwa

Isaac Kamali alikuwa amehukumiwa kifo na mahakama Rwanda, bila hata hivyo kuhudhuria kesi yake mnamo mwaka 2003, lakini adhabu hii "ilifutwa" kwa sababu ya mabadiliko katika sheria ya Rwanda, kulingana na malalamiko ya SCRC . Walakini, aliendelea kulengwa na vyombo vya sheria vya Rwanda.

Mnamo 2008, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Paris wa Roissy-Charles-de-Gaulle wakati akirudi kutoka Marekani na Kigali iliomba Ufaransa kumkabidhi, ombi lililofutiliwa mbali na mahakama ya Ufaransa, kama ilivyofanya kwa watuhumiwa wote waliohusika katika mauaji ya kimbari yaliyodaiwa na Rwanda.

Uchunguzi wa kimahakama ulifunguliwa mnamo 2009 huko Paris baada ya malalamiko ya CPCR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.