Pata taarifa kuu

Upinzani Burundi walalama wafuasi wao kutekwa

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa, amesema anaguswa na mtukio ya kutekwa nyara kwa viongozi wa chama chake, akitolea mfano tukio la Ijumaa ya wiki iliyopita ambapo kiongozi wa chama chake kwenye kitongoji cha Mutimbuzi jijini Bujumbura, Elie Ngomirakiza.

Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa, Julai 27 mwaka 2015.
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa, Julai 27 mwaka 2015. AFP PHOTO / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rwasa, Elie alitekwa nyara na watu wasiofahamika ambao walikuwa katika gari ya kijeshi.

 

Taarifa ya chama hicho inasema, Elie alitekwa wakati alipokuwa akitoka kwenye eneo lake la kazi kupeleka matofali ya kujengea kwa mmoja ya wateja wake mjini Bujumbura.

 

Msemaji wa chama Therence Manirambona, amesema “kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, ilikuwa ni gari ya jeshi, ambayo namba zake tulizipata kuwa ni A031, gari likiwa linamilikiwa na mmoja wa wanajeshi wa Serikali”.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walifanikiwa kumtambua mwanajeshi aliyehusika kumchukua Elie kuwa ni Luteni kanali Aaron Ndayishimiye, anayeongoza kikosi cha 212 kilichoko Rukoko, jirani na mpaka wa DRC, ambapo aliambatana na maofisa wengine wawili wa Serikali za mitaa ambao walimuonesha Elie alipokuwa.

 

Chama hicho kimesema tangu wakati huu hawana taarifa zozote kuhusu mahali Elie Ngomirakiza alipelekwa, na kwamba wameomba vyombo vya usalama kuchukuza mazingira ya kutekwa kwake.

 

Msemaji wa chama ameongeza kuwa walijaribu kumtafuta katika vituo vya polisi vilivyokaribu na eneo alikochukuliwa bila mafanikio na wanahofu kuwa huenda watekaji wanalengo la kumuua.

 

Rwasa, amesema licha ya kuingia kwa utawala mpya wa rais Evariste Ndayishimiye, wafuasi wa chama chake na viongozi wao bado wameendelea kufuatiliwa na vyombo vya usalama, akidai hata ofisi za chama chao kwenye maeneo mbalimbali ya nchi zimeendelea kuchambuliwa.

 

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kitendo cha wafuasi wao kuendelea kutekwa kunadhihirisha kuwa bado hakuna uvumilivu wa kisiasa kwenye taifa hilo.

 

Hadi kufikia sasa wanaharahakati 30 wamekamatwa na wengine zaidi ya 7 hawajulikani walipo katika kipindi cha majuma matatu pekee yaliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.