Pata taarifa kuu

Ajali mbaya ya treni Ugiriki: Maelfu ya waandamanaji wamiminika mitaani Athenes

Karibu watu 10,000 wameandamana Jumapili hii, Machi 5 katikati mwa Athenes, mbele ya makao makuu ya Bunge la Uigiriki, siku tano baada ya ajali mbaya ya trei mbili zilizogongana uso kwa uso.

Baada ya saa moja na nusu ya maandamano, makabiliano yalizuka katikati mwa mji mkuu wa Uigiriki Jumapili hii, Machi 5.
Baada ya saa moja na nusu ya maandamano, makabiliano yalizuka katikati mwa mji mkuu wa Uigiriki Jumapili hii, Machi 5. AP - Yorgos Karahalis
Matangazo ya kibiashara

Baada ya saa moja na nusu ya maandamano, makabiliano yalizuka katikati mwa mji mkuu wa Uigiriki kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama. Hapo awali, waandamanaji waliangusha mamia ya mipira nyeusi kutoa heshima zao kwa wawtu  57 waliofariki katika ajali hiyo mbaya katika hostoria ya nchi hii ya Ulayakwenye njia inayounganisha Athenes na Thesaloniki, huko kaskazini.

Wakati huo Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis alikiri kosa mapema Jumapili asubuhi kwa kuomba msamaha hadharani.

"Kama Waziri Mkuu, ninakiri kosa kuwa serikali inahusika kwa ajali hii, lakini pia ninaomba msmahahasa kwa familia za waathiriwa," ameandika katika anwani ya kawaida. "Katika nchi hii ya Ugiriki ya 2023, haiwezekani kwamba treni mbili zinatembelea kwenye nji moja na kwamba hakuna mtu anayeigundua." "Hatuwezi, hatutaki na sio lazima kujificha nyuma ya kosa la kibinadamu" analohusishwa msimamizi wa kituo, "amebainisha.

'Unafiki'

Lakini katika umati wa waandamanaji, mwalimu Mariana Chronopoulou hakufurahishwa na msamaha huu. Kwa upande wake, anaona kuwa ni "unafiki". "Ikiwa viongozi wangelijali sana maisha yetu, ajali hii isingetokea. Makosa haya mengi ya njia ya reli yangerekebishwa. Viongozi walijua kulikuwa na tatizo la treni. tatizo hilo linadumu miaka kadhaa limekuwa tatizo sugu tangu mgogoro wa kiuchumi, "amsema mwalimu huyu.

Ukosefu wa uzoefu wa mkuu wa kituo cha treni umekosolewa tangu siku moja baada ya ajali hii. Kulingana na vyombo vya habari vya Uigiriki, alipata mafunzo mafupi kabla ya kujikuta mwenyewe, kama msimamzi wa kituo, wakati kulikuwa na shughuli nyingi kwenye barabara hii siku chache kabla ya ajali hiyo kutokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.