Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Equatorial Guinea yagaragazwa kwa mabao 3-0

Vurugu, lawama na huzuni zilitanda wakati wa mchuano wa pili wa nusu fainali kati ya wenyeji Equitorial Guinea na Ghana katika uwanja wa Malabo kufuzu katika hatua ya fainali kutafuta ubingwa wa Afrika.

Kipa wa Ghana Razak Braimah akilindiwa usalama na polisi ya Equatorial guinea, baada ya kuzuka vurugu katika mchuano kati ya Ghana na wenyeji Equatiorial Guinea katika michuano ya Afcon 2015 ya nusu fainali.
Kipa wa Ghana Razak Braimah akilindiwa usalama na polisi ya Equatorial guinea, baada ya kuzuka vurugu katika mchuano kati ya Ghana na wenyeji Equatiorial Guinea katika michuano ya Afcon 2015 ya nusu fainali. FP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Katika mchuano huo wa Alhamisi usiku wiki hii, Ghana walipata ushindi wa mabao 3 kwa 0 na kufuzu katika hatua ya fainali na sasa watamenyana na Cote d'Ivoire siku ya Jumapili Februari 8.

Mchuano huo ulisitishwa kwa dakika 30, baada ya mashabiki wa Equiotoarial Guinea kuanza kuwavamia na kuwashambulia mashabiki wa Ghana kwa kuwarushia chupa za maji, mawe na vifaa vilivyoelezwa kuwa hatari kwa usalama.

Vurugu zilianza baada ya Ghana kupewa penalti katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza na kutiwa kimyani na Jordan Ayew.

Wachezaji wa Ghana waliokuwa nje ya uwanja walilazimika kukimbia na kwenda kujificha nyuma ya goli lao wakiwa pamoja na mashabiki wao ili kuepuka kushambuliwa na mashabiki wa Equatorial Guinea wakiwa nyumbani waliokuwa na hasira.

Helikopta ilionekana ikiuzunguka uwanja wa soka na wakati wa tukio hilo, uwanja wa Malabo ulikuwa kama eneo la vita huku polisi wa kupambana na gahsia wakitumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratsiha mashabiki wa nyumbani.

Baada ya utulivu kurejea refarii kutoka Gabon, Eric Otogo, alichezecha mechi hiyo kwa dakika kadhaa tu kabla ya kuutamatisha.

Kocha wa Ghana, Avram Grant amesema baada ya vurugu hapo jana kwamba anahofia usalama wa wachezaji wake pamoja na mashabiki wa Ghana.

Viongozi wa Shirikisho la soka barani Afrika watakutana Ijumaa wiki hii kujadili na kuthamini vurugu zilizotokea hapo jana.

Equitorail Guinea Jumamosi wiki hii watameyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutafuta mshindi wa tatu.

Fainali ya Cote d'Ivoire na Ghana itakuwa kama ile ya mwaka 1992, ambapo Cote d'Ivoire walishinda kwa penalti 11 kwa 10 baada ya kutoka sare kwa muda wa dakika 120.

PICHA ZINAZOONESHA JINSI HALI ILIVYOKUA KATIKA UWANJA WA MALABO

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.