Timu ya taifa ya Tunisia yakabiliwa na vikwazo
Timu ya taifa ya Tunisia nayo huenda ikachukuliwa hatua na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, baada ya wachezaji kumvamia refarii baada ya kukamilika kwa mchuano wa robo fainali kati yake na Equitorial Guinea.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Katika mchuano huo, wenyeji Equatorial Guinea walipata ushindi wa mabao 2 kwa 1 na kufuzu katika hatua ya nusu fainali.
Viongozi wa CAF walikutana jana Jumatatu na kujadili suala hilo baada ya wachehaji wa Tunisia kulalamika kuwa refarii aliwapa wenyeji penalti ambayo haikustahili katika dakika za lala salama za mchuano huo.
Beki wa Equitorial Guinea Sipoto huenda naye akafungiwa na CAF kucheza katika hatua ya nusu fainali baada ya kuoneakana akimtemea mate mchezaji wa Tunisia.