Pata taarifa kuu

Kenya: Hatukubaliani na uamuzi wa ICJ kuhusiana na mpaka wa baharini na Somalia

Kenya imelaani na kukataa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu haki ICJ, kufuatia uamuzi wake kwa kiasi kubwa kuipendelea Somalia katika mzozo wake wa eneo la mpaka wa Bahari Hindi.

Kenyatta amesema, uamuzi wa Mahakama hiyo utaharibu uhusiano kati ya nchi yake na Somalia na kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kijamii, kiuchumi na kisiasa na anataka sintofahamu hiyo kutataliwa kidiplomasia.
Kenyatta amesema, uamuzi wa Mahakama hiyo utaharibu uhusiano kati ya nchi yake na Somalia na kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kijamii, kiuchumi na kisiasa na anataka sintofahamu hiyo kutataliwa kidiplomasia. Ludovic MARIN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta kwenye taarifa yake, amelaani uamuzi wa Mahakama hiyo, yenye makao yake mjini Hague na kusema serikali yake inakataa kwa nguvu zote uamuzi huo na kusisitiza kuwa kama kiongozi wa nchi Kenya, atahakikisha kuwa mipaka ya eneo hilo la Bahari inalindwa kama ambavyo imekuwa tangu mwaka 1979.

Aidha, Kenyatta amesema, uamuzi wa Mahakama hiyo utaharibu uhusiano kati ya nchi yake na Somalia na kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kijamii, kiuchumi na kisiasa na anataka sintofahamu hiyo kutataliwa kidiplomasia. 

“Kenya inaendelea kushinikiza suluhu ya Kidiplomasia kutatua sintofahamlu hii, kwa hivyo Wakenya wenzangu, niwahakikishie kuwa kama rais wenu, kuwa tuna nia ya kutatua suala hili kwa maelewano, nawaomba muwe watulivu, wakati huu tunapoendelea kutathmini kwa kina suala hili.” amesema rais Kenyatta.

 Naye rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmoja, akilihotubia taifa kupitia Televisheni amesema nchi yake imekubali uamuzi wa Mahakama hiyo na kuitaka Kenya, kuheshimu uamuzi wa Mahakama ili kuimarisha tena uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

 “Kenya inastahili kuona uamuzi wa Mahakama kama fursa ya kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili. Somalia haikuchagua kuwa jirani na Kenya, lakini yalikuwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu ili tuishi kwa amani na jirani zetu. Somalia ilidhamiria hilo siku zote na inalikaribisha hilo.” amesema rais Farmajo.

 Kesi hiyo ilihusu pembetatu ya kilomita za mraba 38,000 katika Bahari ya Hindi ambayo inaaminiwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi. Tayari Kenya ilikuwa imekata kibali kwa kampuni ya nishati ya ENI kutoka Italia kuanza kunza shughuli za upatikanaji wa rasilimali hiyo, hatua ambayo iliikera Somalia.

Uamuzi wa Mahakama hiyo ya ICJ hauwezi kukatiwa rufaa, lakini chombo hicho cha sheria hakina namna ya kutekeleza maamuzi yake. Haifahamiki mpaka sasa kitakachotokea baada ya Kenya kusema haitambui Mahakama hiyo na uamuzi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.