Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Afcon 2015: DRC yajiandaa kumenyana na Cote d'Ivoire

Leo ni siku ya maandalizi ya timu za taifa za soka za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Cote d'Ivoire kujiandaa kwa mchuano wa nusu fainali, kuwania taji la ubingwa wa Afrika.

Mchezaji wa Equatorial Guinea, Javier Balboa, mchezaji wa DRC, Jeremy Bokila, mchezaji wa Cote d'Ivoire, Yaya Toure na mchezaji wa Ghana Asamoah Gyan (kuanzia kushoto kwenda kulia).
Mchezaji wa Equatorial Guinea, Javier Balboa, mchezaji wa DRC, Jeremy Bokila, mchezaji wa Cote d'Ivoire, Yaya Toure na mchezaji wa Ghana Asamoah Gyan (kuanzia kushoto kwenda kulia). REUTERS/Hutchings & Abdallah Dalsh - AFP / DE SOUZA –Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa Jumatano Februari 4 katika uwanja wa Bata nchini Equatorial Guinea kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Maashariki sawa na saa tatu usiku saa za Afrika ya Kati.

Mataifa haya mawili yalimenyana mwaka uliopita katika mechi ya kufuzu kucheza fainali hizi, DRC walifungwa mabao 2 kwa 1 nyumbani na walipokwenda Abidjan waliwafunga Cote d'Ivoire mabao 4 kwa 3.

Hii ni wazi kuwa mechi haitakuwa rahisi Jumatano wiki hii, na kocha wa Leopard Florent Ibenge atakuwa anataka kudhirihisha kuwa ana uwezo wa kuiongoza timu yake kufika fainali, sawa na Mfaransa Herve Renard ambaye lengo lake ni kuhakikisha kuwa Cote d'Ivoire inanyakua taji hilo walilonyakua mwisho mwaka 1992.

Nusu fainali ya pili itakuwa siku ya Alhamisi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea katika uwanja wa Malabo.
Mshambualiaji wa Ghana, Asamoah Gyan anauguza jeraha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.