Pata taarifa kuu
KENYA SOMALIA DIPLOMASIA

Somalia : Kenya yaweza fungua ubalozi wake Mogadishu

Taifa la Somalia limesema Kenya iko huru kufungua tena ubalozi wake nchini Somalia, na kurejesha rasmi shughuli za kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.

Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo akisalimiana na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, hapa ilikuwa jijini Nairobi, tarehe 23 Machi 2017.
Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo akisalimiana na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, hapa ilikuwa jijini Nairobi, tarehe 23 Machi 2017. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua ambayo imejiri siku mbili tu baada ya Kenya, kufungua tena anga yake kwa taifa la Somalia baada ya mafurufuku ya mwezi moja, Somalia ikisema sasa hakuna kinachozuia mataifa hayo mawili kuejesha vikamilifu mahusiano yao ya Kidiplomasia.

Kupitia ujumbe uliotumwa kwa serikali ya Kenya, na waziri wa mambo ya nje wa Somalia, Abdirizak Mohamed, amesema, ‘

kwa mara ya pili chini ya mwezi moja, Kenya, imeonesha  nia ya kuendelea kushirikiana na Somalia, na kumaliza mzozo wa ambao umekuwepo kwa miezi sita.

 

Kutokana na hilo Serikali ya Somalia inaalika Kenya Kufungua tena ubalozi wake Mogadishu, na vilevile sisi tutafungua wetu kule Nairobi.

Mahusiano tata

Kurejeshwa kwa mahusiano kati ya mataifa haya mawili huenda ndio mwanzo wa kumaliza shtuma ambazo zimekuwepo kati yao, Somalia ikilaumu Kenya kwa kuingilia maswala yake ya ndani, madai ambayo Kenya imekuwa ikikanusha vikali.

Hii ina maana kuwa balozi wa Kenya nchini Somalia, Meja jenarali Lucas Tumbo, anaweza rejeshea Mogadishu, sawa na balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Nur Tarzan, kurejea Nairobi.

Wengi sasa wanasubiri kuona iwapo mataifa hayo mawili yatarejesha vikamilifu uhusiano wao wa Kidiplomasia ikizingatiwa kuwa wanajeshi wa kenya miongoni mwa jeshi la Africa linalohudumu nchini Somalia (AMISOM).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.