Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika-AFCON 2015

Afcon 2015: Cote d'Ivoire yachekelea kilio kwa Ghana

Cote d”ivoire imeibuka mshindi wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika iliyokua ikichezwa Equatorial Guinea, kupitia mikwaju ya penalti, baada ya kutoka sare ya kutofungana na Ghana katika muda wa dakika 120.

Kolo Toure akinyanyua Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya mafanikio ya timu yake katika fainali dhidi ya Ghana.
Kolo Toure akinyanyua Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 baada ya mafanikio ya timu yake katika fainali dhidi ya Ghana. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Cote d'Ivoire imebuka mshindi baada ya miaka ishirini na tatu ya kutwa taji hilo ilipoifunga Ghana nchini Senegal mwaka 1992.

Baada ya dakika 120 ya mchezo timu hizo mbili ziliingia katika mikaju ya penalti, ambapo Cote d'Ivoire ilishindwa mikwaju miwili ya kwanza ya penalti, huku Ghana ikiingiza mikwaju miwli ya kwanza ya penalti.

Hata hivyo Ghana ilikuja kushindwa baadae mikwaju miwili ya penalti, na hatimaye kuwa sawa kwa mabao na Cote d'Ivoire (0-0, 8-8). Kutokana na hali hiyo ilibidi magoli kipa kutoka timu mbili wapimane nguvu ikiwa ndio bahati ya mwisho kwa moja ya timu hizo. Kipa wa Ghana alishindwa kuingiza baada ya kipa wa Cote d'Ivoire, Barry, kuokoa jahazi, na baadae kipa huyo wa Cote d'voire kufaulu kuliona lango la mwenziye na kuipa ushindi timu yake ya taifa (0-0, 9-8).

André Ayew ashindwa kuvumilia

Mchezaji nyota wa Ghana, André Ayew alishindwa kujizuia na kuanza kuangusha kilio. Hervé Renard, kocha wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire, ambaye anamjua vema kijana huyo, alijaribu kumtuliza, bila mafanikio. André Ayew, ambaye anaichezea klabu ya Marseille ya Ufaransa, aliingia katika basi lake baada ya saa moja, huku akiendelea kutokwa na machozi.

Mashabiki wa timu ya Ghana walielezea masikitiko yao kuona Ghana inafungwa katika mchuano huo, wakati walikua na matumaini ya kutwa Kombe hilo la Afcon 2015, huku mashabiki wa Cote d'Ivoire wakichekelea na kuimba nyimbo za kuwakatisha tamaa mashabiki wa Ghana. " baba na mwana wamefungwa", waliimba mashabiki wa Cote d'Ivoire. Hata baba wa André Ayew, alipata pigo kama hilo mwaka 1992, baada ya kusimamishwa na kukosa kushiriki katika mchuano wa fainali dhidi ya Cote d'Ivoire.

Yaya Touré afurahia ushindi

Ukweli tulisema kila mara, Yaya Touré, nyota wa Cote d'Ivoire amesema usiku wa jana. " Tulitukanwa sana, wakati mwingine tulifanyiwa vitisho", amesema Yaya Toure. "Wakati unaposhindia klabu, unakua na furaha ya kawaida, lakini unaposhindia timu yako taifa unakua furaha isiyokua na kikomo", ameongeza Yaya Touré.

" Nina furaha sana kwa wananchi wote wa Cote d'Ivoire, ambao walisubiri kwa ushindi huu kwa miaka 23. Ujumbe wangu tangu tulipoanza maandalizi Januari 5 ulikua ni ule ule, hata wakati tulianza vibaya kipindi cha kwanza cha mchezo dhidi ya Guinea, tulikua hatunaa hofu yoyote, tulikuwa tukiambiana baadhi ya ukweli . Wachezaji walionesha uwezo wao, na matunda yameonekana," amesema kocha wa zamani wa Zambia, mabingwa wa Afrika mwaka 2012.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.