Pata taarifa kuu

WHO yatarajia kuwa na uwezo wa kupeleka msaada Tigray katika 'siku chache zijazo'

Shirika la Afya Duniani (WHO) linatumai kwamba msaada wake unaweza kuwasili katika "siku chache zijazo" katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, katika hali ya vita mbaya kwa miaka miwili.

Wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu wakipeleka dawa Mekelle, mji mkuu wa Tigray. Januari 26, 2022.
Wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu wakipeleka dawa Mekelle, mji mkuu wa Tigray. Januari 26, 2022. via REUTERS - INTERNATIONAL COMMITTEE OF THE R
Matangazo ya kibiashara

"Tunatumai kuwa na uwezo wa kuwapa chakula, dawa za muhimu, kurejesha vituo vya matibabu na vifaa vya matibabu, kuwapa watoto chanjo za kimsingi na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yanayozidi kuwa mbaya," afisa huyo alisema. Shirika la Umoja wa Mataifa lilituma barua pepe kwa AFP.

Waasi na mamlaka ya shirikisho la Ethiopia siku ya Jumamosi walikubaliana "kuwafikia wale wote wanaohitaji msaada wa kibinadamu" huko Tigray.

Tangazo hili linafuatia makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mnamo Novemba 2 huko Pretoria (Afrika Kusini), hususan kupokonya silaha kwa vikosi vya waasi, kurejeshwa kwa mamlaka ya shirikisho huko Tigray na uwasilishaji wa misaada. "Watu wanahitaji msaada wa haraka ili kuzuia vifo na mateso zaidi," WHO ilisisitiza.

Mnamo Novemba 9, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, mwenyewe mzaliwa wa Tigray, alikuwa ameomba msaada wa "haraka" wa chakula na matibabu kutumwa katika eneo la Tigray. "Baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano, nilitarajia chakula na dawa vifike mara moja. Sivyo ilivyo," alisema wakati huo.

"Hebu tupe nafasi ya amani, lakini pia tunahimiza usambazaji wa haraka wa chakula na dawa na pia kufunguliwa kwa huduma za msingi kama benki, mawasiliano ya simu na huduma zingine kama umeme, (...) na, kusema ukweli, kuruhusu waandishi wa habari. kama wewe kwenda Tigray,” ameendelea.

"Unaweza kufikiria watu wengi wanakufa kwa magonjwa yanayotibika. Watu wengi wanakufa njaa. Hata katika mapigano, raia wanahitaji chakula na dawa. Hilo haliwezi kuwa hali," alisisitiza.

Baada ya kutengwa na ulimwengu kwa zaidi ya mwaka mmoja, wakaazi milioni sita wa Tigray wanakosa kila kitu: mafuta, chakula, dawa, mawasiliano au umeme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.