Pata taarifa kuu

Ugiriki: Ishirini na sita wafariki na 85 kujeruhiwa katika ajali ya treni

Watu Ishirini na sita wamefariki baada ya treni ya mizigo kugongana na na treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kati ya Athens na Thessaloniki, Ugiriki. Watu 85 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea Jumanne jioni, Februari 28, kikosi cha Zima moto kimetangaza.

Ajali ya treni iliyotokea jioni ya Jumanne Februari 28, 2023 nchini Ugiriki, karibu na Larissa. Treni ya mizigo iligongana na treni iliyobeba abiria 350. Tathmini ya awali iliripoti watu 16 waliofariki na 85 kujeruhiwa.
Ajali ya treni iliyotokea jioni ya Jumanne Februari 28, 2023 nchini Ugiriki, karibu na Larissa. Treni ya mizigo iligongana na treni iliyobeba abiria 350. Tathmini ya awali iliripoti watu 16 waliofariki na 85 kujeruhiwa. AP - Vaggelis Kousioras
Matangazo ya kibiashara

"Takriban watu 26 wamepatikana wamekufa kufikia sasa," afisa wa kikosi cha Zima moto nchini Ugiriki amesema katika mkutano na waandishi wa habari, akiongeza kuwa shughuli ya uokoaji bado inaendelea.

Lakini kulingana na vyombo vya habari vya Ugiriki, ni "ajali mbaya zaidi ya treni ambayo Ugiriki imewahi kupata". Mabehewa matatu yaliacha njia dakika chache kabla ya saa sita usiku Jumanne jioni karibu na jiji la Larissa, katikati mwa nchi, baada ya treni ya mizigo kugongana na treni nyingine iliyokuwa na abiria 350, aliripoti msemaji huyu.

Maafisa wa  kikosi cha Zima moto wapatao 150, pamoja na magari 40 ya wagonjwa mahututi, wametumwa katika eneo la tukio kulingana na idara ya huduma za dharura nchini Ugiriki. "Sijawahi kuona kitu kama hicho katika maisha yangu yote. Inasikitisha. Saa tano baadaye, tunapata miili, "amesema mmoja wa waokoaji ambaye amekuwa anajaribu na timu yake kutoa miili ya abiria iliyokwama ndani ya mabehewa.

Moja ya mabehewa, nyeupe na bendi ya bluu na nyekundu, iliharibika kabisa, na kufanya kazi ya waokoaji kuwa ngumu. Moshi mkubwa na miali ya moto ilikuwa ikitoka kwenye mabehewa mengine.

Abiria waliokwama

"Abiria wengi wamewekwa mahali salama," msemaji wa idara ya zima moto amehakikishia. "Operesheni ya kuwaokoa watu walionaswa inaendelea na inafanyika katika mazingira magumu, kutokana na uzito wa ajali kati ya treni hizo mbili," amesema pia.

Moja ya mabehewa hayo yalishika moto na watu kadhaa walinaswa, kulingana na kituo cha televisheni cha umma cha Ert. Katika kituo cha televisheni cha Skai, Gavana wa mkoa huo, Kostas Agorastos, ametangaza kwamba "zaidi ya abiria 250 walihamishwa kwa basi kwenda Thessaloniki", jiji la pili la nchi, kaskazini.

"Kwa bahati mbaya idadi ya waliojeruhiwa na waliofariki huenda ikawa kubwa," ameonya. Waziri wa Afya Thanos Plevris ametembelea eneo la tukio wakati Waziri wa Mambo ya Ndani Takis Theodorikakos anasimamia hali hiyo kutoka kituo cha kudhibiti mgogoro akiambataa na wakuu wa polisi na maafisa wa kikosi cha zima moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.