Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Moto waendelea kuteketeza mali na vitu karibu na Athens

Moto unaoendelea kuathiri Ugiriki unaendelea kushika kasi katika maeneo ya karibu na mji wa Athens Jumamosi hii, na kupelekea mamlaka kuwahamisha mamia ya wakaazi katika maeneo salama.

Helikopta inajaza maji kutoka Ziwa Beletsi wakati moto wa misitu ukizuka karibu na kijiji cha Ippokratios Politia, kaskazini mwa Athens, Ugiriki Agosti 6, 2021.
Helikopta inajaza maji kutoka Ziwa Beletsi wakati moto wa misitu ukizuka karibu na kijiji cha Ippokratios Politia, kaskazini mwa Athens, Ugiriki Agosti 6, 2021. REUTERS - COSTAS BALTAS
Matangazo ya kibiashara

Kwenye Mlima Parnes, nje kidogo ya mji mkuu wa Ugiriki, moto uliosababishwa na upepo mkali na joto kali pia umesababisha maelfu ya watu kuohamishwa.

Kama ilivyo katika nchi zingine za Mediterania, hali ya hewa ni kali msimu huu wa joto nchini Ugiriki, wimbi la joto ambalo halijawahi kutokea katika zaidi ya miongo mitatu ikiwa imesababisha moto wa wakati mmoja nchini kote.

Kyriakos Mitsotakis, Waziri Mkuu wa Ugiriki, amesikitiswa na "majira ya joto kali" na kuahidi kuwa serikali yake itaendelea katika mstari wa mbele katika kulinda maisha ya biadamu.

Zaidi ya maafisa 700 wa kikosi cha zima moto, kutoka Ugiriki, Kupro, Israel na Wafaransa wamepelekwa kaskazini mwa Athens kupambana na moto huo, na msaada kutoka kwa jeshi na washambuliaji wa maji.

Katika nchi jirani ya Uturuki, mamlaka zinapambana na moto mbaya zaidi wa misitu ambao nchi haijawahi hiyo haijawahi kushuhudia, na makumi ya maelfu ya watu, ikiwa ni pamoja na watalii, wamelazimika kuhamishwa. Nchini Italia, upepo mkali ulisababisha moto katika mji wa Sicily wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.