Pata taarifa kuu

Ugiriki yaidhinishiwa kiasi cha pesa na Umoja wa Ulaya kujikwamua kiuchumi

Nchi ya Ugiriki, hivi leo imekuwa taifa latatu kwenye Jumuiya ya Ulaya, kuidhinishiwa kiasi cha pesa kitakachosaidia taifa hilo kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya mpango wa umoja wa Ulaya kusaidia nchi wanachama kukabiliana na makali ya covid 19.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, Januari 29, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, Januari 29, 2020. REUTERS/Benoit Tessier/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume ya ulaya, Ursula von der leyen, amesema kiasi cha fedha kitakachotolewa kwa Ugiriki, kitasaidia pakubwa kuinusuru nchi hiyo na mdororo zaidi wa kiuchumi, baada ya nch za Hispania na Ureno, kuidhinishiwa mpango wao hapo jana.

Msaada huu wa kifedha unatoka katika kiasi cha Euro bilioni 750 kilichopitishwa na nchi wanachama za ulaya kuyasaidia mataifa yaliyoathirika pakubwa na virusi vya corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.