Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Mwandishi wa habari wa Ugiriki, mtaalam wa maswala ya jinai, auawa Athenes

George Karaivaz, anayejulikana sana kwa Wagiriki, alipigwa risasi na kuuawa Ijumaa Aprili 9 alipokuwa akirudi nyumbani kwake nje kidogo ya mji mkuu Athenes. Shambulio hilo, ambalo limezua hofu kwa raia wa Ugiriki, lilitekelezwa na watu wawili walio kuwa kwenye pikipiki ambao walimpiga risasi mara 15.

Lori la polisi limebeba gari la mwandishi wa habari Giorgos Karaïvaz, aliyeuawa kwa kupigwa risasi wakati akishuka kwenye gari lake katika viunga vya Athenes, Aprili 9, 2021.banlieue d'Athenes, le 9 avril 2021.
Lori la polisi limebeba gari la mwandishi wa habari Giorgos Karaïvaz, aliyeuawa kwa kupigwa risasi wakati akishuka kwenye gari lake katika viunga vya Athenes, Aprili 9, 2021.banlieue d'Athenes, le 9 avril 2021. AP - Panayiotis Tzamaros
Matangazo ya kibiashara

“Ni huzuni kwetu sote. Hivi ndivyo msemaji wa serikali ya Ugiriki alivyoelezea mauaji ya mwanahabari Giorgos Karaivaz. "Shambulio la demokrasia," kimesema chama cha upinzani cha Kinal. Aina hii ya mauaji ni "kitendo kibaya na cha ujinga," Ursula von der Leyen, rais wa Tume ya Ulaya, amebaini kwenye Twitter.

Giorgos Karaïvaz, aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wawili kwenye pikipiki Ijumaa, alikuwa ni baba wa familia. Ameacha mke na watoto wawili. Aliuawa papo hapo, aliposhuka kwenye gari lake, baada ya kurudi kutoka kazini.

Mwandishi wa habari alijulikana sana kwa Wagiriki kwa ushiriki wake kwa ukweli aliyokuwa akitoa katika makala ya ZINA ya kila siku kwenye kituo cha runinga cha Star TV. Giorgos Karaïvaz, 50, pia alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa Bloko, wavuti ambayo masuala ya ufisadi yalikuwa muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.