Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UTURUKI-USALAMA-USHIRIKIANO

Ugiriki: Mazungumzo kati ya Athenes na Ankara yaendelea kukumbwa na sintofahamu

Katika eneo la mashariki mwa Mediterania, hali ya sintofahamu bado inaendelea kati ya majirani wawili, Ugiriki na Uturuki, nchi ambazo zimekuwa zikifanya mazoezi ya kijeshi kwenye bahari hiyo wiki hii.

Meli za Uigiriki zinashiriki katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Italia, Ufaransa na Kupro kwene bahari ya mashariki ya Mediterania, Agosti 25, 2020.
Meli za Uigiriki zinashiriki katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Italia, Ufaransa na Kupro kwene bahari ya mashariki ya Mediterania, Agosti 25, 2020. Handout / GREEK DEFENCE MINISTRY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Suala la uchimbaji wa rasilimali ya gesi katika eneo hilo limeongeza hali ya sintofahamu kati ya nchi hizo mbili. na kama hakuna mazungumzo yoyote kuna hatari ya kuzuka makabiliano zaidi.

Mazungumzo kwa minajili ya kuzuia kutumbukia kwenye mzozo wazi ni moja wapo ya mambo muhimu kati ya Athene na Ankara. Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani siku ya Jumanne wiki hii katika miji mikuu ya nchi hizo mbili haijazaa matunda yoyote kwa kuanza kwa mazungumzo hayo. Siku ya Jumatano jioni, rais wa Marekani, alimpgia simu Waziri Mkuu wa Ugiriki, akimtaka kuanzisha mazungumzo na Uturuki, wito ambao mpaka sasa bado haujaitikiwa.

Ugiriki inasema iko tayari kupunguza shinikizo la kijeshi na uwezekano wa kushiriki mazungumzo, ikiwa Uturuki itasitisha 'mara moja' kile ambacho athenes inaita "uchochezi".

Kwa upande wake rais wa Uturuki Recep Erdogan amesema kwamba Uturuki itasimama kidete kutetea haki zake za Bahari ya Mediterania, huku akiIhimiza Ugiriki kuepuka mzozo.

Erdogan amesema Uturuki iko tayari kufanya kila liwezekanalo kuchukuwa haki yake iliopo katika Bahari ya Mediterania, pia Bahari ya Egean na Bahari Nyeusi. Ameiomba Ugiriki kubaki kando ya mzozo huo.

Jumatano, Waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis alisisitizia nia ya kuweko na mazungumzo baina ya nchi yake na Uturuki kuhusu mipaka ya eneo maalum la kiuchumi kwenye eneo la mashariki la Mediterania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.