Pata taarifa kuu
UGIRIKI-EU-UTURUKI-WAHAMIAJI-USALAMA

EU yaahidi kusaidia Ugiriki kukabiliana na ongezeko la wakimbizi

Umoja wa Ulaya utasaidia Ugiriki kukabiliana na kuongezeka kwa wakimbizi kutoka Uturuki, rais wa Tume ya umoja huo Ursula von der Leyen ameahidi Jumanne wiki hii.

Pamoja na rais wa baraza la Ulaya Charles Michel na spika wa bunge la Ulaya David Sassoli, rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen atafanya tathimini ya hali ilivyo katika mpaka huo wa kaskazini mashariki wa Orestiada.
Pamoja na rais wa baraza la Ulaya Charles Michel na spika wa bunge la Ulaya David Sassoli, rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen atafanya tathimini ya hali ilivyo katika mpaka huo wa kaskazini mashariki wa Orestiada. REUTERS/Francois Lenoir/Pool/File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Hali kwenye mpaka wetu sio suala la Ugiriki peke yake. Usimamizi ni jukumu la Ulaya kwa ujumla," Ursula von der Leyen amewaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake yeye pamoja na viongozi wa Ulaya na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika eneo hilo.

"Wale ambao wanaonekana kujaribu umoja wa Ulaya wataambulia patupu. Tutaendelea kujidhatiti, na umoja wetu utatawala (...) Wasiwasi wa Ugiriki pia unagusa Ulaya", rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, ameongeza.

Wakati huo huo rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anaendelea kuongeza shinikizo na kutishia kufungua mipaka yake kuwaruhusu wahamiaji na wakimbizi kutoka Syria wanaotafuta hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Kiasi ya wahamiaji 13,000 wamekwama wakijaribu kuvuka na kuingia katika mataifa ya umoja wa Ulaya kutoka Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.