Pata taarifa kuu
UGIRIKI-WAHAMIAJI-USALAMA

Ugiriki: Wakimbizi 1,800 wahamishwa kwenda katika kambi mpya ya Kara Tepe

Polisi katika Kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki, wanawahamisha maelfu ya wahamiaji kutoka katika kambi yao ya awali ya Moria, iliyoteketetea moto.

Tangu kuzuka kwa moto huo, maefu ya wakimbizi wapatao Elfu 12 wamekuwa wakilala nje kwenye baridi bila ya chakula, makaazi na maji.
Tangu kuzuka kwa moto huo, maefu ya wakimbizi wapatao Elfu 12 wamekuwa wakilala nje kwenye baridi bila ya chakula, makaazi na maji. REUTERS/Elias Marcou
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ugiriki imesema kuwa wakimbizi 1,800 wanahamishwa kwenda katika kambi mpya katika mji wa Kara Tepe.

Maafisa wa usalama wapatao sabini wameonekana wakienda kuzuru eneo jpya ambalo wahamiaji hao wataanza maisha mapya, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Siku ya Jumatano, wahamiaji kutoka Afgaistan walishtuliwa kuanzisha moto huo wiki iliyopita.

Tangu kuzuka kwa moto huo, maefu ya wakimbizi wapatao Elfu 12 wamekuwa wakilala nje kwenye baridi bila ya chakula, makazi na maji.

Licha ya harakati hizo za serikali ya Ugiriki, baadhi ya wakimbizi wamekataa kuondoka katika kambi ya Lesbos, na wanataka kwenda katika nchi nyingine barani Ulaya, wengi wakitamani Ujerumani.

Kabla ya kuwasili katika kambi hiyo mpya, wahamiaji hao wanapimwa maambukizi ya Corona na tayari, watu 56 wemepatina na maambukizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.