Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGIRIKI-UTURUKI-USALAMA-USHIRIKIANO

Kyriakos Mitsotakis: Ugiriki haiwezi kufanya mazungumzo na Uturuki 'chini ya kitisho cha bunduki'

Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukuwa vikwazo "muhimu" dhidi ya Uturuki isipokuwa pale Ankara itasitisha uwepo wake wa baharini mashariki mwa Mediterania, amesema Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika mahojiano yaliyochapishwa Alhamisi wiki hii.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, Januari 29, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, Januari 29, 2020. REUTERS/Benoit Tessier/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ugiriki inaendelea katika mvutano na Uturuki kuhusiana na maliasili ya gesi na mafuta pamoja na ushawishi wa jeshi la majini katika eneo la mashariki mwa Mediterania ambao umezusha hofu za mzozo.

Suala hilo litakuwa kiini cha mkutano wa nchi za kusini mwa Umoja wa Ulaya, ambao Ufaransa inaandaa Alhamisi hii huko Ajaccio.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakuwa mwenyeji wa viongozi wa mataifa yanayopakana na bahari ya Mediterania kwa mkutano unapapangwa kuzungumzia hali ya wasi wasi kati ya Uturuki na mataifa ya mashariki mwa bahari hiyo.

Lengo la mazungumzo hayo ni "kupiga hatua katika kupata muafaka juu ya uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Uturuki ikiwa pamoja na yote kabla ya mkutano wa Septemba 24-25 wa Umoja wa Ulaya," afisa wa ofisi ya rais wa Ufaransa amesema.

"Tunahitaji mazungumzo, lakini sio kwa bunduki," ameandika Kyriakos Mitsotakis.

"Kinachohatarisha usalama na utulivu wa nchi yangu kinatishia ustawi na usalama wa nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya", ameongeza Waziri Mkuu wa Uigiriki katika mahojiano yaliyochapishwa na magazeti ya Frankfurter Allgemeine Zeitung la nchini Ujerumani, Le Monde la nchini Ufaransa na The Times la London.

Mkutano huo katika kisiwa cha Ufaransa cha Corsica kitawaleta pamoja viongozi wa Ufaransa, Italia, malta, Ureno na Uhispania pamoja na wanachama wa Umoja wa Ulaya wa mataifa ya mashariki mwa bahari ya Mediterania Ugiriki na Cyprus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.