Pata taarifa kuu

Sudan: Omar Bashir amehamishiwa kwenye kituo cha ulinzi mkali wa jeshi

Nairobi – Wakili wa rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir, amesema mteja wake ameondolewa hosipitalini ambako amekuwa tangu kuzuka kwa mapigano kwenye taifa hilo mwezi Aprili mwaka uliopita na kuhamishiwa katika êneo la ulinzi mkali linalolindwa na jeshi.

Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir.
Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir. REUTERS - Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Mohamed al-Hassan al-Amin aliiambia tovuti ya habari ya Sudan Tribune kwamba kiongozi huyo wa zamani, pamoja na watu wengine wanne, wamehamishwa kutoka katika kituo hicho cha matibabu baada ya huduma za afya huko kutatizika pakubwa.

Bashir, ambaye alikuwa amehukumiwa kwa makosa ya ufisadi, alikuwa pia akikabiliwa na kesi ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1989, na alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya kijeshi katika mji wa Omdurman ambayo ulizingirwa na wapiganaji wa RSF.

Washirika wa kikanda na kimataifa wa Sudan wameshindwa kupatanisha jeshi na RSF katika vita ambavyo vimesababisha vifo vya takriban watu 14,000 na wengine milioni 10 kutoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.