Pata taarifa kuu

Raia wawili wa Guinea wapigwa risasi na kufariki wakati wa maandamano

Vijana wawili wamepigwa risasi na kuuawa siku ya Jumatatu katika viunga vya Conakry wakati wa siku ya kwanza ya mgomo mkuu uliolenga kupinga utawala wa kijeshi tangu mwaka 2021, shirika la habari la AFP limeripoti likinukuu vyanzo vya familia na hospitali.

Barabara kuu ya Fidel Castro ilikuwa tupu, kwenye lango la Kaloum, mjini Conakry, Jumatatu hii, Februari 26, 2024.
Barabara kuu ya Fidel Castro ilikuwa tupu, kwenye lango la Kaloum, mjini Conakry, Jumatatu hii, Februari 26, 2024. Β© Matthias Raynal / RFI
Matangazo ya kibiashara

"Wamemuua mtoto wetu, wamemlenga na kumpiga risasi shingoni," Adama Keita, kijana wa miaka 18 ambaye alinaswa katika mapigano hayo na vikosi vya usalama, mwanajeshi ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameliambia shirika la habari la AFP. "Niliuona mwili wa kijana huyu, machozi yalinibubujika, na mara moja niliondoka eneo la tukio ili nisihusishwe na aina hii ya uhalifu," ameongeza mwanajeshi ameongeza.

Kijana mwingine alifariki katika mazngira kama hayo, daktari katika hospitali ya John Paul II alikofariki ameliambia shirika la habari la AFP. Tovuti ya habari ya Guineematin.com iliweza kumhoji babake kwa njia ya simu, Aboubacar TourΓ©, ambaye amethibitisha kifo hicho.

"Mnamo saa 12 jioni, walinipigia simu nikiwa eneo la ujenzi kuniambia kuwa walimpiga risasi mtoto wangu. Nikiwa njiani kuelekea nyumbani, mdogo wangu alinipigia simu kuniambia kuwa amefariki," amesema. Mamadi Doumbouya alipoingia madarakani alisema haki itakuwa dira itakayowaongoza Waguinea wote, leo hii anafanya vibaya kuliko yule mwingine (Alpha CondΓ©), mbaya zaidi ya yule, mbaya zaidi ya yule mwingine,” amesema baba wa kijana huyo, aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya mtandaoni.

Siku ya kwanza ya mgomo mkuu iliitikiwa na watu wengi nchini Guinea. Shughuli mbalimbali zilizorota katika mji mkuu wa Conakry siku nzima. Maduka, shule, benki zimefungwa, mitaa ilikuwa tupu. Mapigano yamezuka mara kwa mara katika baadhi ya maeneo katika vitongoji vya mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.