Pata taarifa kuu

Guinea: Utawala wa kijeshi wavunja serikali iliyokuwepo tangu mwaka 2022

Nairobi – Utawala wa kijeshi nchini Guinea, hapo jana umetangaza kuivunja Serikali iliyokuwepo tangu mwaka 2022 na kwamba inatarajiwa kutangaza safu mpya ya uongozi katika siku chache zijazo.

Kiongozi wa Guinea kanali Mamadi Doumbouya, Tarehe 22 Septemba 2022.
Kiongozi wa Guinea kanali Mamadi Doumbouya, Tarehe 22 Septemba 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Ni tangazo lililosomwa kwenye runinga ya kitaifa na afisa mkuu wa Utawala wa kijeshi nchini humo, Brigedia Jenerali Amara Camara, tangazo lililowahstua wengi wa wananchi na wadau.

Hata hivyo haijabainika nini sababu za kuvunjwa kwa serikali iliyoteuliwa tangu Julai 16, 2022, na aliyekuwa waziri mkuu Bernard Goumou aliyechukua nafasi ya Mohamed Béavogui, ambaye alilazimika kuondoka ofisini kwa sababu za kiafya.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, agizo la rais Mamady Doumbouya, linasema kuanzia Jumatatu ya Februari 19 ni makatibu wa baraza la mawaziri na wasaidizi wao wakuu ndio wamepewa jukumu la kushughulikia shughuli zote za serikali.

Tangu kuingia madarakani kwa kiongozi huyo baada ya mapinduzi ya Septemba 5, 2021 Serikali, ilikuwa imefanyiwa mabadiliko machache mno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.