Pata taarifa kuu

Rais wa zamani Ernest Bai Koroma aondoka Sierra Leone kuelekea Nigeria

Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma, aliyeshtakiwa kwa madai ya kuhusika katika matukio ya Novemba 26 yaliyoelezwa kama "jaribio la mapinduzi ya serikali" na serikali, ameondoka nchini mwake siku ya Ijumaa, ndugu zake wawili wamesema.

". Bw Koroma alishtakiwa mapema mwezi wa Januari kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na uhaini na kuficha uhaini. Tangu mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, alikuwa amewekwa chini ya masharti ya kutotembea sawa na kifungo cha nyumbani.
". Bw Koroma alishtakiwa mapema mwezi wa Januari kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na uhaini na kuficha uhaini. Tangu mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, alikuwa amewekwa chini ya masharti ya kutotembea sawa na kifungo cha nyumbani. © Michèle Spatari / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Bw. Koroma, 70, alipata idhini kutoka kwa mahakama siku ya Jumatano kwenda nchini Nigeria kwa muda usiozidi miezi mitatu kwa matibabu. Hii ni "ishara ya kibinadamu", alisema Mkuu wa Nchi Julius Maada Bio Alhamisi jioni wakati wa hotuba kwa taifa.

Kwa mujibu wa Sheriff Mahmud Ismail, mshauri wa Bw. Koroma, mkuu wa zamani wa nchi (kutoka 2007 hadi 2018) alipanda ndege ya jeshi la Nigeria, bila kutaja hatua ya mwisho ya safari yake. Afisa kutoka chama chake ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina kwamba Bw. Koroma ameondoka kwenye makazi yake kuelekea Nigeria.

Kulingana na vyombo vya sheria vya Sierra Leone, Mahakama iliidhinisha rais huyo wa zamani kupata matibabu nchini Nigeria "kwa muda usiozidi miezi mitatu kuanzia tarehe ya agizo hili lilipotoleana (kwa sharti) kwamba wadhamini wake watoe masasisho ya mara kwa mara ya matibabu, yaliyotiwa saini na kuidhinishwa.

Mapema Novemba 26, watu kadhaa waliojihami kwa bunduki za kivita walishambulia ghala la kijeshi, kambi mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, wakikabiliana na vikosi vya usalama. Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21: askari 14, maafisa wa polisi, askari magereza, maafisa wa usalama, mwanamke mmoja na washambuliaji watatu.

Takriban watu 80 walikamatwa kuhusiana na matukio haya, hasa askari, 27 kati yao wanashitakiwa kwa "uasi". Bw Koroma alishtakiwa mapema mwezi wa Januari kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na uhaini na kuficha uhaini. Tangu mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, alikuwa amewekwa chini ya masharti ya kutotembea sawa na kifungo cha nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.