Pata taarifa kuu

Wakuu wa IGAD wanakutana nchini Uganda kujadili mizozo ya Pembe ya Afrika

Nairobi – Wakuu wa nchi za ukanda wa IGAD wanakutana nchini Uganda hivi leo kwenye kikao kisichokuwa cha kawaida, kujadili namna ya kutatua mizozo inayoendelea kwenye nchi za pembe ya Afrika za Sudan, Somalia na Ethiopia.

Wakuu wa nchi za IGAD
Wakuu wa nchi za IGAD © IGAD
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu uliitishwa na rais wa Djibouti, Ismaïl Omar Guelleh, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya IGAD, kujadili namna ya kumaliza vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF na mvutano wa kidiplomasia kati ya Somalia na Ethiopia, baada ya uongozi wa Addis Ababa kuingia kwenye makubaliano ya kijeshi na matumizi ya Bahari na jimbo linalojitawala la Somaliland.

Djibouti's president, Ismaïl Omar Guelleh, has been at the helm of the tiny strategic state since 1999
Djibouti's president, Ismaïl Omar Guelleh, has been at the helm of the tiny strategic state since 1999 AFP/File

Hata hivyo, mkutano huo hauteahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, ambaye amesema ana majukumu mengine mazito yasiyoweza kuahirishwa, wakati huu kukiwa na ripoti kuwa huenda akazuru mji mkuu wa Somaliland Hargeisa, baada ya kuingia kwenye mkataba huo, suala ambalo litachochea zaidi mvu tano wake na Somalia .

Naye kiongozi wa kijeshi wa Sudan Janerali Abdel Fattah al-Burhan, hatakuwa kwenye kikao hicho baada ya kuishtumu IGAD kwa kumwalika kiongozi wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemetti.

Utawala wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,umekuwa ukipambana na kundi na RSF nchini Sudan
Utawala wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhan,umekuwa ukipambana na kundi na RSF nchini Sudan © AFP PHOTO / HO/ SAUDI PRESS AGENCY

Wataalam wa masuala ya diplomasia wanasema hatua ya Jenerali Burhan, ni kama kujipiga risasi mguuni, kwa sababu anajitenga na jirani zake.

Viongozi wa IGAD wanatarajiwa kuja na mapendekezo, wanayosema yatakubali na pande zote ili kusitisha vita vilivyoanza mwezi Aprili mwaka uliopita na kusababisha viveo vya zaidia ya watu Elfu 13 na kuwaacha mamilioni bila makaazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.