Pata taarifa kuu

Watu watatu wauawa katika shambulizi la kujitoa mhanga mjini Mogadishu

Takriban watu watatu waliuawa na wawili kujeruhiwa siku ya Jumanne katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga karibu na ofisi ya meya katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kulingana na polisi na mashahidi.

Mogadishu mara kwa mara hulengwa na mashambulizi ya kundi la wanajihadi la Al Shabab, ambalo limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, kwa zaidi ya miaka 16.
Mogadishu mara kwa mara hulengwa na mashambulizi ya kundi la wanajihadi la Al Shabab, ambalo limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, kwa zaidi ya miaka 16. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji, ambaye pia aliuawa, alilipua bomu nje ya mgahawa, polisi imesema katika taarifa. "Kati ya waathiriwa, kuna watatu waliokufa na wawili kujeruhiwa," polisi imeongeza. Walioshuhudia wanasema waliona mshambuliaji wa kujitolea mhanga akiwakimbia polisi kabla ya mlipuko huo.

Gari lililokuwa limeegeshwa karibu lilishika moto baada ya mlipuko huo, amesema shahidi Mohamud Halane. "Watu wameshtuka," amesema, akiongeza kuwa miili ilikuwa imelala chini. Shambulio hilo halikudaiwa mara moja na kundi lolote.

Mogadishu mara kwa mara hulengwa na mashambulizi ya kundi la wanajihadi la Al Shabab, ambalo limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho ya Somalia, inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, kwa zaidi ya miaka 16. Waasi hawa wanaohusishwa na Al-Qaeda walidhibiti mji mkuu hadi mwaka 2011, walipofukuzwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika. Lakini Al Shabab bado imeanzishwa katika maeneo makubwa ya vijijini katikati na kusini mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.