Pata taarifa kuu

Mechi za AFCON kuanza leo nchini Ivory Coast

Nairobi – Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. 

Mashindano ya AFCON yameanza nchini Ivory Coast
Mashindano ya AFCON yameanza nchini Ivory Coast © RFI/FMM
Matangazo ya kibiashara

Ni saa za kuhesabu hapa Abidjan , kabla ya kuanza kwa mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Coite Dvoire na Guinea-Bissau kwenye uwanja wa Allasane Outtara. 

Kuanzia mapema leo, mashabiki wa soka, hasa wa hapa Cote Dvoire walianza kufurika uwanjani, kuishabikia timu yao, iliyoshinda mara mwisho taji hili mwaka 2015. 

Serikali ya Cote Dvoire, imewahakikishia usalama wageni wote waliokuja kutazama michuano hii, na maafisa wa polisi na wanajeshi zaidi ya Elfu 17 wanatumiwa kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa. 

Mbali na hapa Abidjan, michuano hii itakayomalizika Februari 11, inachezwa pia kwenye jiji kuu  Yamoussoukro, Bouake, mji wa Pwani wa  San Pedro, Korhogo uliopo Kaskazini. 

Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. 

Jason Sagini, Abidjan, RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.