Pata taarifa kuu

Sudan: Mkuu wa jeshi amewatembelea wanajeshi wake jijini Khartoum na Omdurman

Nairobi – Nchini Sudan, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel fatah al burhan, amewatembelea  wanajeshi wake katika kambi mbili za kimkakati jijini Khartoum na Omdurman, ziara aliyofanya saa chache tangu kundi la RSF lidhibiti kambi kubwa ya Nyala.

Al Burhan, ametupilia madai kuwa makao makuu ya jeshi kwenye mji wa Darfur na miji jirani yamechukuliwa na wapiganaji wa RSF
Al Burhan, ametupilia madai kuwa makao makuu ya jeshi kwenye mji wa Darfur na miji jirani yamechukuliwa na wapiganaji wa RSF AP - Aron Ranen
Matangazo ya kibiashara

Televisheni ya taifa ilirusha picha za video zikimuonesha jenerali al Burhan akisalimiana na wanajeshi katika kambi za Wadi Seidna iliyoko Omdurman na ile ya Karari iliyoko Khartoum.

Aidha Al Burhan, ametupilia madai kuwa makao makuu ya jeshi kwenye mji wa Darfur na miji jirani yamechukuliwa na wapiganaji wa RSF, akisisitiza kuwa na udhibiti.

Jenerali Burhan pia amewakashifu wapiganaji wa RSF kuendeleza mashambulio dhidi ya ngome za jeshi licha ya mazungumzo yanayoendelea mjini Jeddah, kiongozi huyu akisisitiza yuko tayari kwa suluhu ya kudumu.

Mazungumzo yanayoratibiwa na Saudi Arabia, Marekani, Au na jumuiya ya IGAD, yanalenga kuzishawishi pande zinazohasimiana kusitisha mapigano na kusaka suluhu ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.