Pata taarifa kuu

Zaidi ya vifo 200 kutokana na homa ya Dengue vyarekodiwa tangu Januari 1 nchini Burkina Faso

Mlipuko wa homa ya Dengue, ugonjwa unaoenezwa na mbu, umeua watu 214 nchini Burkina Faso tangu Januari 1, hasa katika mji mkuu wa Ouagadougou na Bobo-Dioulasso, mji wa pili wa nchi hiyo, serikali ya Burkina Faso imetangaza siku ya Alhamisi.

Mbu hatari wa simbamarara ndiye msambazaji wa virusi kama Chikungunya, Zika au Dengue.
Mbu hatari wa simbamarara ndiye msambazaji wa virusi kama Chikungunya, Zika au Dengue. © Shutterstock _ InsectWorld
Matangazo ya kibiashara

"Tunakumbusha kuwa kuanzia Januari 1 hadi Oktoba 15, 2023, jumla ya wagonjwa 50,478 wanaoshukiwa kuambukizwa homa ya Dengue ziliripotiwa, ikijumuisha wagonjwa 25,502 wanaowezekana na vifo 214," serikali imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari, huku ikisisitiza kwamba "kwa kipindi pekee kuanzia Oktoba 9 hadi 15, 2023, idadi ya wagonjwa10,117 wanaoshukiwa kuambikizwa ilirekodiwa, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 4,377 wanaowezekana na vifo 48".

Mlipuko wa Dengue bado unaendelea katika miji miwili ilikoanzia: Ouagadougou na Bobo-Dioulasso", kulingana na Waziri wa Afya, Robert Lucien Jean-Claude Kargougou.  Amebainisha kwamba mlipuko wa Dengue unaambatana na mlipuko wa ugonjwa mwingine unaoambukizwa na mbu uitwao Chikungunya tangu mwezi Septemba.

"Tangu Septemba hadi wiki iliyopita tumerekodi wagonjwa 207 waliothibitishwa katika nchi yetu", lakini hakuna vifo, amesema Bw. Kargougou. "Ili kukabiliana vyema na hali hii ya afya, baadhi ya hatua zimechukuliwa, ikiwa ni pamoja na vipimo vya uchunguzi wa haraka katika vituo vya afya vya umma," amesema.

Kampeni ya kunyunyizia dawa za mbu pia imezinduliwa katika miji miwili iliyoathiriwa zaidi. Burkina Faso imekuwa na wagonjwa wa homa ya Dngue tangu miaka ya 1960, lakini mlipuko wa kwanza ulirekodiwa kutoka 2017, na vifo 13.

Dengue inaenezwa na kuumwa na mbu aliyeambukizwa, kama vile Malaria inavyoonyesha dalili zilezile, ni virusi vinavyoenea katika nchi zenye joto jingi, ambavyo hutokea hasa mijini na nusu mijini, na kusababisha watu milioni 100 hadi 400 wanaambukizwa kila mwaka , kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Homa ya Dengue inaweza kusababisha Homa kali, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kutapika, maumivu ya misuli na, katika hali mbaya zaidi, kutokwa na damu, hali ambayo inaweza kusababisha kifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.