Pata taarifa kuu

Homa ya ndege: Namibia yasitisha uagizaji wa kuku wa Afrika Kusini

Namibia imesitisha uagizaji wa kuku na mayai kutoka kwa jirani yake Afrika Kusini, katika kukabiliana na mlipuko mbaya zaidi wa homa ya ndege katika historia yake, serikali ya Namibia imetangaza siku ya Jumatano.

Homa ya mafua ya ndege kwa ujumla ni ya msimu lakini katika miaka ya hivi karibuni kesi zimeonekana mwaka mzima.
Homa ya mafua ya ndege kwa ujumla ni ya msimu lakini katika miaka ya hivi karibuni kesi zimeonekana mwaka mzima. © AP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unakuja baada ya ongezeko "la kutisha" la visa vya "homa ya ndege yenye kusababisha magonjwa mengi", imesema Wizara ya Kilimo ya nchi hii ya kusini mwa Afrika. "Uagizaji na usafirishaji" wa kuku hai, nyama ya kuku, mayai na vifaranga kutoka Afrika Kusini umesitishwa, kulingana na chanzo hicho.

Mmoja wa wazalishaji wakuu wa kuku barani Afrika, Afrika Kusini iliripoti visa vya kwanza vya mafua ya ndege kwenye mashamba mwezi Aprili. Kwa sababu ya ukaribu wake, Afrika Kusini ilikuwa "muuzaji mkuu" wa kuku kwa Namibia. Lakini nchi hiyo pia inaagiza kuku kutoka Ulaya na Amerika Kusini, msemaji wa Wizara ya Kilimo ya Namibia Jona Musheko ameliambia shirika la habari la AFP.

Wiki iliyopita, wafugaji wa kuku nchini Afrika Kusini walionya juu ya tishio la uhaba wa kuku katika miezi ijayo kutokana na homaa hii mbaya. Kampuni ya Quantum Foods, mojawapo ya makampuni makubwa, ilielezea masikitiko yake kwa kupoteza katika mashamba yake hadi kufikia dola milioni 5.3 (euro milioni 4.9), au kuku milioni mbili, kutokana na virusi hivyo. Mzalishaji mkubwa zaidi nchini, Astral, pia ilitangaza kuwa soko linakabiliwa na uhaba wa mayai.

Ulimwenguni kote, homa ya ndege inaambukiza mamalia ya wanyama, kutoka kwa mbweha hadi simba wa baharini, na hivyo kuongeza hofu kwamba virusi hivyo vitabadilika kuwaambukiza wanadamu kwa urahisi zaidi, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Maambukizi kwa ujumla ni ya msimu lakini katika miaka ya hivi karibuni kesi zimeonekana mwaka mzima, na wataalam sasa wanazingatia milipuko hiyo kuwa mikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.