Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Ituri: Miili 15 ya raia yagunduliwa katika vijiji 3 katika eneo la Irumu

Miili 15 ya raia ilipatikana Jumatatu Agosti 7 katika msitu karibu na vijiji vya Samboko, Makutano na Mutweyi Aodi kusini mwa eneo la Irumu katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, radio Okapi nchini humo imechapisha kwenye tovuti yake.

Wanajeshi wa Kikosi cha jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) wakishika doria katika moja ya maeneo ya mkoa wa Ituri.
Wanajeshi wa Kikosi cha jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) wakishika doria katika moja ya maeneo ya mkoa wa Ituri. Abel Kavanagh MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wa haki za binadamu wanashutumu waasi wa ADF kwa kuwaua raia hao Jumamosi ya wiki iliyopita katika vijiji hivi vinvyopatikana kwenye barabara kati ya Komanda na Luna.

Waaharakati hao wameiomba mamlaka kupeleka timu ya waokoaji kwenye eneo la tukio ili miili hiyo iweze kuzikwa kwa heshima.

Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la CRDH, Christophe Munyaderu, amesema kuwa raia wengine watano walichukuliwa mateka na wauaji hao.

Ameomba uingiliaji kati wa haraka wa jeshi la DRC, FARDC, kukomesha ukatili wa ADF katika eneo hili ambapo watu wengi waliohamishwa wamekuwa wakirejea vijijini mwao kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia utulivu ambao umekuwa ukiripotiwa.

Christophe Munyaderu pia amependekeza kuandaliwa kwa operesheni kubwa ili kutokomeza vitendo hivi vya ukatili vya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.