Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Islamic State yakiri kuhusika na mauaji ya watu 23 DRC

Raia zaidi ya 23 wameuawa usiku Jumapili kuamkia Jumatatu katika shambulio linalohusishwa kundi la waasi wa Uganda la ADF (Allied Democratic Forces) katika kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vyanzo vya ndani vimebaini.

Wanajeshi wakiwa katika eneo linalokabiliwa na hali tete kiusalama, mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wakiwa katika eneo linalokabiliwa na hali tete kiusalama, mashariki mwa DRC. © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Watu 24, wakiwemo wanawake sita, waliuawa katika shambulio hili la ADF" katika kijiji cha Makugwe, katika eneo la Beni mkoani Kivu Kaskazini, Roger Wangeve, kiongozi wa shirika la kiraia katika eneo hilo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Akiwa ziarani katika kijiji hiki, mbunge wa mkoa Saidi Balikwisha amesema "watu 23 waliuawa" katika shambulio la ADF. Mbunge huyu ameomba idadi ya wanajeshi wenye ujuzi iongezwe na wapewe vifaa vya kutosha kukabiliana na vilivyo na adui".

Kulingana na Roger Wangeve, miongoni mwa waathiriwa ni watu 17 ambao walikuwa "katika baa ndogo ambapo walikuwa wakinywa bia". ADF "waliwaua wote", amesema.

Angalau nyumba saba za makazi zilichomwa moto, maduka matatu ya dawa na maduka kumi na moja kuporwa, wakati idadi "ya raia waliopelekwa msituni bado haijajulikana", ameongeza Bw. Wangeve. "Tunasikitika na tunajiuliza swali: itawezekanaje kuua raia mita chache kutoka kambi ya jeshi?", ameshangaa.

Akihojiwa na shirika la habari la AFP, Kanali Charles Omeonga, mkuu wa wilaya ya Beni, amebaini kwamba wanajeshi "wanawawinda adui" ambaye, "anajificha kati ya raia".

Kundi la ADF, waasi wa Kiislamu wenye asili ya Uganda, wanaendesha harakati zao kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini na kusini mwa jimbo jirani la Ituri. Kundi hili lenye silaha, lililotangazwa na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS) kama tawi lake katikati mwa Afrika, ni mojawapo ya makundi mabaya zaidi katika eneo la mashariki mwa DRC.

Shambulio kubwa la mwisho la kundi hili lilitokea Januari 15 wakati watu wasiopungua 14 waliuawa na wengine 63 kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika kanisa la Kipentekoste. ADF iliwekwa mnamo 2021 na Marekani katika orodha yake ya "mashirika ya kigaidi ya kigeni", yenye uhusiano na IS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.