Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Takriban watu 10 wauawa katika shambulizi la ADF Ituri

Takriban raia kumi wameuawa na waasi wa ADF kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, duru za ndani zimesema Jumatano ambazo zimkosoa operesheni ya pamoja ya majeshi ya Kongo na Uganda katika eneo hilo.

Jeshi la DRC, FARDC,  linaendelea na mashambulizi dhidi ya kundi la waasi wa Uganda ADF katika mkoa wa Ituri.
Jeshi la DRC, FARDC, linaendelea na mashambulizi dhidi ya kundi la waasi wa Uganda ADF katika mkoa wa Ituri. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Watu hawa kumi - wanawake wawili na wanaume wanane - waliuawa Jumanne wakati wa uvamizi ulioongozwa na wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF) katika kijiji cha Ndalya, katika wilaya ya Irumu kusini mwamkoa wa Ituri, Christophe Munyanderu, kiongozi wa shirika lisilo la kiserikali la CRDH, ameliambia shirika la habari la AFP.

Chanzo kingine kimetaja idadi ya vifo ambayo haijathibitishwa ya watu 14. Washambuliaji hao pia waliteketeza nyumba mbili na pikipiki moja. Jumatano asubuhi, Bw. Munyanderu ameongeza, mwanajeshi mmoja wa DRC alijeruhiwa baada ya kukanyaga "bomu lililotengenezwa kienyeji lililowekwa mita 500 kutoka barabara ya taifa namba 4" ambayo wapiganaji wa ADF walikaribia, wakilenga vijiji vinavyokaribu na barabara hiyo.

Siku ya Jumanne, waasi kumi na moja wa ADF waliuawa nchini Uganda baada ya kuvuka mpaka kutoka DRC, kulingana na jeshi la Uganda. Tangu mwishoni mwa mwezi wa Novemba 2021, majeshi ya DRC (FARDC) na Uganda (UPDF) yamekuwa yakifanya operesheni za pamoja kujaribu kuwazuia waasi wa kundi hili la waasi wa Uganda.

Bw. Munyenderu anasema operesheni hizi hazikuzaa "matunda yoyote yaliyotarajiwa na raia". Baada ya wiki chache za utulivu, mauaji yameanza tena, anajutia Dieudonné Malangai, mwanaharakati wa mashirika ya kiraia kutoka katika eneo Walese Vonkutu, ambako kijiji cha Ndalya kinapatikana.

"Tunasikitika kwamba oparesheni za pamoja kati ya FARDC na UPDF hazikuwahi kufanyika katika eneo letu, bado askari wa Uganda wako karibu na Boga na Tchabi", vijiji viwili jirani, amesema.

"Ndalya sio eneo letu tunapaswa kuwajibika, askari wetu bado hawajawekwa kwenye barabara ya kitaifa nambari 4", amejibu luteni kanali Mak Hazukay, msemaji wa operesheni hizi za pamoja, akihojiwa na shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.