Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Idadi ya vifo yaongezeka baada ya shambulio la bomu katika kanisa la Kiprotestanti Kasindi

Idadi ya vifo imeongezeka baada ya shambulio lililotokea Januari 15, 2023 huko Kasindi, eneo la Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kanisa la Kiprotestanti ndilo lililolengwa na shambulio la bomu wakati wa ibada ya Jumapili. Kulingana na wakuu wa jeshi na mashirika ya kiraia watu 14 waliuawa na 63 kujeruhiwa.

Kundi la Islamic State nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limekiri kuhusika katika shambulio la bomu kanisani huko Kasindi.
Kundi la Islamic State nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limekiri kuhusika katika shambulio la bomu kanisani huko Kasindi. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Dharura kwa sasa ni kuwaondoa waliojeruhiwa vibaya zaidi. Kulingana na mashirika ya kiraia ya Kasindi, karibu watu 30 wanahitaji kuhamishwa haraka hadi katika hospitali ya ICRC huko Beni, kilomita 75 kutoka eneo la shambulio.

Magari kadhaa ya wagonjwa mahututi ya kijeshi yamekuwa yakibea majeuhi hadi katika hospitali ya shirika la ICRC. Inachukua karibu saa mbili kufika Beni. Dharura, kwa sababu Kasindi inakosa dawa za kuwatibu majeruhi hawa. Afisa mmoja wa shirika la kiraia anaeleza kuwa hospitali hiyo haitoi huduma ya kutosha kwa majeruhi na kwamba jana walilazimika kuzunguka kwenye maduka ya dawa kutafuta dawa za kuwatibu waathirika. Siku ya Jumatatu Hifadhi ya dawa ilikuwa inakaribia kuisha.

Hata kama kundi la ADF mara kwa mara litafanya mashambulizi, halijawahi kufanya shambulio kanisani, amebaini mtafiti Thierry Vircoulon kutoka Taasisi ya Uhusiano ya Kimataifa ya Ufaransa (Ifri).

Hili sio shambulio la kwanza la bomu kuhusishwa ADF katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Kulikuwa na mashambulio kadhaa katika mwaka 2022. Ni lazima kusema kwamba ni shambulio la kwanza ambalo linalenga kanisa.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.