Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Raia wa Kenya akamatwa kwa kuhusishwa na shambulio kanisani

Mamlaka nchini DRC inamshikilia raia wa Kenya anayeshukiwa kuwa mwanachama wa waasi wa ADF wanaotuhumiwa kutekeleza shambulio kanisani ambako watu 10 walifariki Kivu Kaskazini Jumapili.

Wanajeshi wa DR Congo wakipiga doria mashariki mwa taifa hilo
Wanajeshi wa DR Congo wakipiga doria mashariki mwa taifa hilo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la DR Congo Kapteni Anthony Mualushayi amesema mshukiwa alikamatwa katika kituo cha mpaka cha Kasindi muda mfupi baada ya shambulio hilo kutokea.

Congo haijaweka wazi jina la mshukiwa huyo aliyekamatwa Jumapili japokuwa kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Kenya (ATPU) kimemtambua kama Abdirizak Muktar Garad, mwenye umri wa miaka 29, anyetokea katika kaunti ya Wajir kaskazini mwa Kenya.

Mamlaka nchini DRC imeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wote waliohusika katika shambulio hilo.

Watu 17 waliripotiwa kufariki katika shambulio hilo watu wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa.

Waasi wa ADF wanaendelea kuwa tishio kwa usalama wa raia wanaoishi mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.