Pata taarifa kuu

Sudan: Kiongozi wa RSF amemtaka mkuu wa jeshi na washirika wake kujiuzulu

Nairobi – Nchini Sudan, kiongozi wa wanamgambo wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, sasa anataka Mkuu wa Majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na washirika wake wa karibu wajiuzulu, ili vita vinavyoendelea viishe.

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan (Kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo maarufu kama Hemedti (Kulia).
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan (Kushoto) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo maarufu kama Hemedti (Kulia). © AP
Matangazo ya kibiashara

Wito huu wa Jenerali Daglo, ameutoa kupitia mkanda wa video, ujumbe wake unaoaminiwa kuwa wa kwanza tangu kuanza kwa vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa miezi mitatu sasa.

Aidha, kiongozi huyo wa RSF amesema kuwa, iwapo Jenerali al-Burhan atajiuzulu, vita vinavyoendelea vitaisha ndani ya saa 72.

Akiwa amevalia magwanda ya kijeshi, huku akizungukwa na wapiganaji wa RSF walionekana wenye furaha, Jenerali Daglo amesisitiza kuwa anataka kuona amani na utulivu vikirejea katika nchi yake.

Licha ya wake wapigano makali yameendelea kushuhudiwa huku wanamgambo wa RSF na jeshi la Sudan wakishambuliana kwa roketi na ndege za kivita katika maeneo yenye watu wengi jijini Khartoum.

Mapigano nchini Sudan yamesababisha vifi vya watu 3900 na wengine zaidi ya Milioni 3.5 wakiyakimbia makaazi yao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.