Pata taarifa kuu
HAKI-DIPLOMASIA

Afrika Kusini: Mvutano kuhusu uwezekano wa Putin kuwasili katika mkutano wa kilele wa BRICS

Afrika Kusini inaendelea na maandalizi yake kabla ya mkutano wa kilele wa BRICS mjini Johannesburg kuanzia Agosti 22 hadi 24. Hata hivyo bado suala la rais wa Urusi kushiriki mkutano huo nchini Afrika Kusini limeendelea kuzua sintofahamu wakati anakabiliwa na waranti wa kimataiafa wa kukamatwa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow, Julai 14, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow, Julai 14, 2023. AP - Alexei Babushkin
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Wiki hii, kumepangwa kufanyika mkutano wa kwanza wa vyama vya siasa vya kambi ya rais na vile vinavyochukuliwa kuwa "washirika" na ANC unapangwa. 

Lakini swali kuu ni ikiwa rais wa Urusi Vladimir Putin atakuja au la, ambaye anakabiliwa na waranti wa kimataifa wa kukamatwa. Kukamatwa katika ardhi ya Afrika Kusini kunaweza kuwa sawa na "tangazo la vita" kwa upande wa rais Cyril Ramaphosa.

Wakati rais wa Afrika Kusini bado anakataa kuzungumza wazi juu ya suala hilo, nyaraka zilizowekwa wazi na mahakama zimezungumzia suala hilo. Afrika Kusini ambayo ni nchi iliyotia saini Mkataba wa Roma, italazimika rais wa Urusi ikiwa atathubutu kuweka mguu wake kwenye ardhi ya Afrika Kusini kushiriki wa mkutano wa BRICS.

Lakini kulingana na Cyril Ramaphosa, "Urusi imeweka wazi kwamba kumkamata rais wake itakuwa tangazo la vita. Na haitakuwa sawa na Katiba yetu kuhatarisha nchi yetu kuingia vitani. Rais wa Afrika Kusini alikuwa akijibu katika hati hizi ombi la chama kikuu cha upinzani nchini humo, ambacho kinajaribu kuhakikisha kuwa mahakama itachukua mkondo wake iwapo Vladimir Putin atahubutu kuingia nchini Afrika Kusini.

Kama Paul Mashatile, makamu wa rais wa Afrika Kusini, alivyoeleza kwa kina katika vyombo vya habari vya ndani, mkuu wa nchi wa Urusi hadi sasa amekataa chaguzi nyingine zinazotolewa na Pretoria, yaani kushiriki mkutano kwa njia ya video au kumuagiza Waziri wake wa Mambo ya Nje. Kuhamishia mkutano huo katika nchi nyingine pia imeshindikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.