Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-HAKI

Afrika Kusini yasumbuka tangu ICC kutoa waranti dhidi ya Vladimir Putin

Afrika Kusini imekuwa na wasiwasi tangu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilipotoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa kwa Vladimir Putin. Kwa sababu Pretoria, iliyo karibu na Moscow na ambayo inakataa kulaani vita nchini Ukraine, inakusudia kumpokea rais wa Urusi katika mkutano wa kilele wa BRICS mwishoni mwa mwezi Agosti. Lakini kama ataingia nchini Afrika Kusini, mamlaka itakuwa na wajibu wa kumkamata: nchi hiyo imetia saini Mkataba wa Roma.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (hapa ilikuwa mwezi Februari 2023) alikataa kulaani vita vya Ukraine vilivyoanzishwa na Urusi.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (hapa ilikuwa mwezi Februari 2023) alikataa kulaani vita vya Ukraine vilivyoanzishwa na Urusi. © Themba Hadebe / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Romain Chanson

Jambo moja lenye uhakika: Afrika Kusini haiwezii kumfunga pingu Rais wa Urusi Vladimir Putin. Kwa hivyo, Pretoria inatafuta nji mbadala ili kutuliza hali joto inayozidui kupanda na inashauriana kutafuta suluhu la mkutano wa BRICS, unaoleta pamoja Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini. Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini amesema anasubiri maoni mapya ya kisheria kuhusu suala hilo, ambaye alikiri kuwa 'ni jambo linalotia wasiwasi'.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kudharau kujiunga na Mkataba wa Roma. Mnamo 2015, Pretoria ilishindwa kumkamata Rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir. Hata hivyo Afrika Kusini ilifikiria kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mwaka 2016.

Chama cha Democratic Alliance, chama cha kwanza cha upinzani kinachounga mkono raia wa Ukraine, kinamtaka Rais Cyril Ramaphosa kuzuia tu kuwasili kwa Vladimir Putin. Hata hivyo, chama chenye msimamo mkali cha Economic Freedom Fighters kinasema kiko tayari kumpokea Putin kwa mikono miwili. "Tunawajua marafiki zetu, tunajua walitusaidi kuwa huru," kiongozi wa chama EFF Julius Malema amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.