Pata taarifa kuu
URUSI-ICC

Nchi ya Urusi nayo yatangaza kujitoa kwenye mahakama ya ICC

Nchi ya Urusi imetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujitoa kwenye mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, ikisema mahakama hiyo imeshindwa kutumiza matumaini ya jumuiya ya kimataifa.

Jengo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC.
Jengo la mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC. REUTERS/Jerry Lampen/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Urusi ilitia saini mkataba wa Roma mwaka 2000, ikiwa ni mahakama ya kwanza ya kudumu ya kidunia kuanzishwa, itakayoshughulikia makosa ya uhalifu wa kivita, lakini hata hivyo haikuwa kuthibitisha mkataba huo.

"Mahakama imeshindwa kufikia matumaini ya jumuiya ya kimataifa kuhusu kuanzishwa kwake na haijawahi kuwa huru," imesema taarifa ya wizara ya mambo ya nje, ambapo imeongeza kuwa "mahakama hiyo imefanya kazi kwa kuegemea upande mmoja."

Utawala wa Moscow unasema kuwa, haujafurahishwa na namna ambavyo kesi yake kuhusu vita fupi iliyohusisha nchi hiyo na majirani zake Georgia mwaka 2008, ukisema mahakama hiyo ilidharau uhalifu uliofanywa na utawala wa Tbilisi dhidi ya raia kwenye eneo la kusini mwa Ossetia, eneo ambalo linaunga mkono utawala wa Moscow.

Russia's President Vladimir Putin addresses the audience during a ceremony of receiving diplomatic credentials from foreign ambassadors at the Kremlin in Moscow, Russia, November 9, 2016. REUTERS/Sergei Karpukhin
Russia's President Vladimir Putin addresses the audience during a ceremony of receiving diplomatic credentials from foreign ambassadors at the Kremlin in Moscow, Russia, November 9, 2016. REUTERS/Sergei Karpukhin Reuters/路透社

"Kwa hali kama hii hakuna anayeweza kuzungumzia kuhusu imani yake na mahakama ya ICC," imesema taarifa ya wizara, ikiongeza kuwa "uamuzi wa kutoshiriki kwenye mkataba wa Roma" ni uamuzi uliochukuliwa na rais Vladmir Putin.

Nchi ya Urusi inakuwa taifa la kwanza kwenye ukanda wa Ulaya kutangaza kujitoa kwenye mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama ya ICC, hatua inayokuja wakati huu kukifanyika kongamano la nchi wanachama wa mkataba wa Roma.

Mbali na Urusi, tayari nchi tatu za Afrika na zenyewe zimeshatangaza kujiondoa kwenye mahakama hiyo, ambapo tayari nchi ya Burundi, Afrika Kusini na Gambia, zimeshawasilisha barua zao kwa baraza la umoja wa Mataifa kulitaarifu kuhusu kujitoa kwao.

Baadhi ya nchi za Afrika zinakosoa utendaji wa mahakama hiyo, zikidai kuwa imekuwa ikiwalenga viongozi wa Afrika peke yake na kuwaacha baadhi ya viongozi wa nchi za magharibi ambao wamehusika katika maujai ya kimbari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.